Hebu someni haya kutoka kwa kocha msaidizi wa Yanga

Na Mwandishi wa Michezo
KOCHA Msaidizi wa timu ya Yanga Charles Mkwasa alianza rasmi kufundisha mazoezi kikosi cha timu hiyo huku akisisitiza suala zima la nidhamu na uwajibikaji.

Mkwasa alichaguliwa kuchukua nafasi ya aliekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo Fred Minziro ambae kwa sasa yeye pamoja na aliyekuwa kocha mkuu Enerst Brandits walipewa mkono wa kwaheri kuifundisha timu hiyo.

Mkwasa akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazoezi na kikosi hicho yaliyofanyika katika uwanja wa Bora Kijitonyama alisema kuwa nidhamu ndio inaweza kuibadilisha Yanga.

Alisema kuwa amepewa timu hiyo kutoka kwa makocha ambao nao walikuwa na uwezo wao lakini anaona kuwa njia kubwa ambayo kwa upande wake anatakiwa kutumia ili kuyafikia mafanikio ni suala zima la nidhamu.

Alisema kuwa wachezaji wanatakiwa kuwa na nidhamu katika mazoezi, ikiwa kuwahi muda kujituma na kuwa makini katika mafunzo.

Alisema kuwa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndio ataendelea na kuchagua kikosi chake cha kwanza kwa kuwa kwa sasa bado anaendelea na kuwasoka wachezaji.

Wakiwa kwenye uwanja huo jana Mkwasa alitumia zaidi ya saa tatu kuwafanyisha mazoezi wachezaji wa kikosi hicho.

Gazeti hili lilimshuhudia kocha huyo akiwa makini zaidi katika kuwalekeza mazoezi ya pumzi, kuumudu mpira pamoja na kufunga.

Akianza na mazoezi ya pumzi wachezaji walianza kwa kukimbia taratibu kuuzunguka uwanja mara  tano.

Baada ya hapo waliendelea kuuzunguka uwanja huku safari hii wakiwa wanakimbia nusu uwanja na kisha kukimbia uwanja mzima mara nane bila ya kupumzika.

Walipumzika kama dakika 15 wakinywa maji baada ya hapo waliendelea tena kuuzunguka uwanja mara 15 huku akiwa anawafuatia kwa nyuma.

Gazeti hili lilimsikia akiwa anawahamasisha kwa kusema "chukulieni kwa sasa ndio zimebakia dakika 10 na mnataka goli mbili haya kimbieni harakaharaka".

Alikuwa pia akiwasisitiza wavute pumzi kuingia ndani na kutoa pumzi nje kwa nguvu.
Hali hiyo iliwafanya washabiki waliokuwa wakifuatilia mazoezi hayo kufurahia huku wengine wakisema kuwa awali wakati wa Brandits wachezaji walikuwa wakifanya mazoezi kidogo na kupumzika.

Mkwasa anaonekana kuwa ameanza akiwa kocha makini zaidi hasa kutokana na namna ambavyo ameanza kwa kukinoa kikosi hicho.

Katika kuthibitisha kuwa hataki mzaha alifikia wakati akasisitiza kuwa atawasiliana na uongozi ili kujua muda mbao wachezaji akina Emanuel Okwi na Khamis Kiiza wamepewa kupumzika na kuhakikisha kuwa anafuatilia kiundani na kuhakikisha kuwa wanawasili klabunihapo haraka.

"Mimi sioni kama inakuwa na muhimu kuona kuwa wachezaji wengi wapo kazini  na wengine bado wanasuasua mimi nataka kuhakikisha kuwa kila kitu kinaenda kama ratiba yangu inavyotaka sitaki kabisa suala la kuchelewa"alisema Mkwasa.

Hata hivyo Afisa Habari wa Yanga Baraka Kiziguto alisema kuwa wachezaji hao waganga wanawasiri leo kutoka nchini kwao.

Wachezaji wengine ambao hawakufika mazoezini ni pamoja na Mrisho Ngasa ambae anaumwa homa ya mapafu (Nimonia) Simon Msuva huku Nadir Haroub, Canavaro alifika mazoezini lakini hata hivyo hakucheza kutokana na mauimivu ya goti.

Yanga kwa sasa inamsaka kocha mkuu ambapo inatarajiwa kuwa awe ameshatambulishwa katika klabu hiyo kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu utakaoanza Januari 25 mwaka huu.

Yanga katika kujiimarisha zaidi kimchezo imelazimika kukwepa kushiriki Kombe la Mapinduzi ili kuimarisha benchi lake la ufundi.
Mwisho

Related

Sanaa 8982180546108304842

Post a Comment

emo-but-icon

item