Kulekea Bunge la Katiba, hali ilivyo sasa huko bungeni Dodoma hebu soma mwenyewe

Hivi sasa kinachoendelea bungeni ni zoezi la kurudia kwa upigaji wa kura katika kuchagua nafasi ya mwenyekiti.

Upigaji wa kura wa mwanzo ulilazimika kusimama na kurudiwa tena upya hiyo ni baada ya wasimamizi wa kuhesabu kura kugundua kuwa kura zimekuwa nyingi kulingana na idadi ya wajumbe wa Bunge hilo

Wapo wabunge waliosema kuwa inatakiwa kura zilizozidi eti zitolewa, hivi hawa inamaana kuwa hata hawajui kuwa kwa kufanya hivyo inaweza kuharibu zoezi zima kwa kuwa itakuwa ni ngumu kujua ni kura gani ingestahili kuwepo au ipi ya kuondoa.

Sasa ikambidi Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe kushauri kuwa inabidi ipigwe kura moja kwa mtu mmoja na kisha wahakikishe kuwa hakuna mtu anajirudia.

Aliongeza kuwa "Hili ni tuki kubwa na lisilotaka uzembe ni tukio la kihistoria tusipokuwa makini na kugawa karatasi za kupigia kura hivyo wapuuzi watarejea na uzembe ule ule na kujikuta tukirudia tena kuoiga kura".

Kwa sasa kinachoendelea bungeni ni kuanza tena upigaji wa kura na wanaenda kupiga kura mtu mmoja mmoja mbele ya meza iliyopo bungeni.

Kikao kinaendeshwa na Mama Oliver Luena ambae ni mjumbe wa Bunge hilo la Katiba.

Kilichoishangaza Blog hii ni hatua ya Tv ya taifa kutoka hewani na kuanza kucheza nyimbo za muziki wa Bongo Fleva wakati kuna masuala muhimu kama haya kwa taifa.

Binafsi nimejikuta nikimkumbuka ghafla aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tv hiyo Tido Muhando kwa kuwa kingechokuwa kikifanyika hadi sasa ingekuwa ni kufanyika kwa mjadala kuhusiana na Bunge hilo kwa watu mbalimbali na sio kuweka muziki.

Tujifunze kutoka kwa wenzetu Kenya ile inaitwa Citizen Tv huwa hawafanyi mzaha katika vitu kama hivi ila wangekuwa wanalifuatilia suala hili seriously.

Tutaendelea kuleta habari ya nini kinaendelea bungeni

Related

Sticky 9010617522782495812

Post a Comment

emo-but-icon

item