Ozil anaweza kutimka--- Wenger

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa hakuna mchezaji yoyote wa klabu hiyo ambae ambae anaweza kutoachwa kutokana na kushindwa kuonesha uwezo katika soka.

Pia amesisitiza kuwa hata mchezaji wake Metsus Ozil anaweza kuachwa pia msimu ujao au hata kabla kutokana na kushindwa kuonesha uwezo kulingana na mkataba wake.


Wenger kwa sasa inasemekana kuwa anaweza kuwaacha baadhi ya wachezaji wake katika kikosi chake hicho.


Mchezaji huyo Ozil amekuwa akinyooshewa vidole kutokana na kushindwa kuonesha uwezo mkubwa kwenye klabu hiyo.


Hivi majuzi alikosa penati katika mchezo dhidi ya timu ya Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi Mbingwa.


Wenger alisema kuwa kuanzia sasa hatosajili mchezaji kutokana na ukubwa wa jina lake ila atazingatia yale masuala muhimu na ya msingi katika mchezo.


Alisema kuwa kitu cha msingi kwake ni kuchukua mchezaji atakaesaidia kushinda kwa mchezo na sio kutoa upendeleo wa aina yoyote


Alisema kuwa katika michezo yake ya sasa iliyobakia atakuwa akiwachezesha wachezaji kwa zamu zamu huku akiangalia uwezo wa kila mmoja unavyokua.


Pia alionesha kufurahishwa na uwezo wa mchezaji wake Yaya Sanogo ambae ameonekana kuwa yupo tayari kuiletea timu hiyo mabadiliko baada ya kuonesha mchezo safi dhidi ya Liverpool na Bayern Munich.


"Mchezaji huyu yupo tayari kupambana na kusaidia mafanikio ya Arsenal na hiyo inaonekana katika mchezo wake na vile anavyoonesha kuwa na shauku ya kazi iliyopo mbele yake"alisema Wenger.


Alisema kuwa anatambua kuwa sio uzoefu pekee ndio utakafanikisha upatikanaji wa mabao lakini pia anaangalia umakini na uwezo binafsi wa mchezaji husika.

Related

Sticky 7455554467117458103

Post a Comment

emo-but-icon

item