Makampuni yatakiwa kujiunga na harakati za Malaria Safe katika kupambana na ugonjwa wa Malaria
https://habari5.blogspot.com/2014/04/makampuni-yatakiwa-kujiunga-na-harakati.html
Lilia Makau kutoka Tanzania Breweries akiwakaribisha wageni |
Awaichi Mawalla from Zantel akifafanua jambo, Zantel ni moja kati ya wadau wakubwa katika vita dhidi ya Malaria hapa nchini |
Wadau wakimsikiliza Awaichi |
Mada ilikuwa ni nzuri sana |
Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Ledeger Tenga akizungumza katika kikao hicho, Tenga ni balozi wa kujitolea wa Malaria |
Waziri Nyoni ambae ni Meneja wa Miradi kutoka John Hopkins University akitoa mada kuhusiana na hali ya ugonjwa Malari nchini |
Makampuni mbalimbali nchini yametakiwa kuwa na utaratibu maalum wa kuwaelimisha wafanyakazi wake kuhusiana na ugonjwa wa Malaria.
Wito huo ulitolewa jana na Meneja Miradi wa Chuo Kikuu cha John Hopkins Waziri Nyoni wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya Malaria duniani.
Nyoni alisema kuwa ili kuhakikisha utendaji mzuri na wenye tija kwa faida ya makampuni hayo na taifa kwa ujumla ni vema wafanyakazi wakaeupuka maambukizi ya ugonjwa wa Malaria ambao ni hatari kwa afya za wafanyakazi hao.
Alisema kuwa kwa sasa ni makampuni 37 tu hapa nchini ambayo yamejiunga na mpango wa upambanaji wa ugonjwa wa Malaria katika sehemu za kazi na tayari faida zake zimeanza kuonekana.
Alisema kuwa kupitia mpango huo wafanyakazi wa makampuni mbalimbali wanapewa elimu bure kuhusiana na ugonjwa wa Malaria kutoka kwa wataalamu wa John Hopkins.
Alisema kuwa inayotolewa na John Hopkins ni kuhusiana na elimu nzima ya ugonjwa huo, namna ya kujilinda na hamasa ya kupambana na ugonjwa huo.
"Sisi kama wataalamu tupo tayari kutoa elimu bure kabisa kuhusiana na ugonjwa huo na namna ya kupambana nao na tupo tayari muda wowote kufika katika mahala hapo pa kazi"alisema Nyoni.
Akizungumzia siku ya Malaria Duniani itakayofanyika Agost 25 mwaka huu alisema kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Wazi ri Mkuu Mizengo Pinda.
Alisema kuwa Waziri Mkuu ni balozi namba moja wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo huku akiwa ameshiriki kikamilifu katika kuhamasisha makampuni kujiunga katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.