Kili Award 2014 ilivyobamba
https://habari5.blogspot.com/2014/05/kili-award-2014-ilivyobamba.html
MWANAMUZIKI wa kizazi kipya Nasib Abdul ametia fora katika tuzo za kili 2014 baada ya kchukua tuzo saba za shindano hilo.
Tukio hilo lilitokea juzi ambapo Diamond aliongoza kwa idadi ya wasanii waliochukua tuzo nyingi huku msanii Farid Kubanda, Fid Q akichukua kwa mara ya kwanza na akachukua tuzo mbili.
Diamond alichukua kipengele cha Mwimbani bora wa kiume, wimbo bora wa kushirikishwa kupitia wimbo wake wa Muziki Gani, pia alishinda kipengele cha kuwa mtunzi bora wa mwaka muziki wa kizazi kipya, Video bora ya mwaka kupitia video yake ya My Number One, wimbo bora wa mwaka pamoja na mtumbuizaji bora wa kiume wa mwaka pamoja na wimbo bora.
Diamond amevunja rekodi iliyowekwa na mwanamuziki 20 percent wa mkoani Morogoro ambae alishinda tuzo tano kwenye tuzo hizo miaka ya nyuma.
Diamond katika tuzo hizo aliwabwaga wasanii wenzake ambao alikuwa akishindanishwa nao ambapo ameshinda katika kila kipengele alichokuwa akishindanishwa na hivyo kuwa ndio msanii alieng'ara siku hiyo.
Pia mbali na kushinda tuzo hizo alitoa burudani ya aina yake baada ya kuimba wimbo wake wa My Number One live na kuwavutia watu wengi waliohudhuria onesho hilo.
Katika tukio jingine lililotokea siku hiyo msanii wa Hip Hop, Fid Q kwa mara ya kwanza alipata tuzo ambapo alichaguliwa kuwa msanii bora wa Hip Hop na mtunzi bora wa mwaka wa muziki huo wa Hip Hop.
Bendi ya Mashujaa nayo iliibuka kidedea kwa kujinyakulia tuzo nyingi, ilichukua tuzo ya wimbo bora wa mwaka bendi kupitia wimbo wake wa ushamba mzigo, bendi bora ya mwaka huku kipengele cha rapa bora wa mwaka bendi akishinda Ferguson.
Kwa upande wa bendi ya Twanga Pepeta iliambulia tuzo moja ambayo ilichukuliwa na mwanamuziki wake Luiza Mbutu alieshinda kipengele cha mwimbaji bora wa kike.
Bendi ya Mapacha wa watatu iliwakilishwa na Jose Mara baada ya kuchukua tuzo ya mwimbaji bora wa kiume.
Mwimbaji wa Taarab Isha Mashauzi alichukua kipengele cha mwimbaji bora wa kike taarab na pia mtumbuizaji bora wa kike wa mwaka.
Mzee Yusuph nae alipata tuzo mbili ambazo ni mwimbaji bora wa kiume taarab na mtunzi bora wa mwaka wa taarabu kwa upande wa wanaume.
Nick wa Pili alifanikiwa kuchukua tuzo ya wimbo bora wa Hip Hop kupitia wimbo wake wa Nje ya Box, mwanamuziki Camereon alishinda katika kipengele cha wimbo wa Tubonge.
Tuzo ya mtunzi bora wa mwaka bendi ilienda kwa Christian Bella.
Kitu kikubwa ambacho kilivutia siku hiyo mbali na mpangilio mzuri wa burudani lakini pia ni mshereheshaji wa tukio hilo Mpoki ambae alichekesha na kupendezesha tukio hilo.
Mpoki alikuwa kivuti kikubwa kutokana na uwezo wake katika kutunga vichekesho vya hapo hapo ambavyo viliwavutia wengi.
Hasa pia kuna muda alimshangaa mwanamuziki Vanessa Mdee kwa kutaka kuondoka akienda kuchukua tuzo na pia alivyokuwa akizungumza kiingereza zaidi.
Mpoki aliropoka" Khaa! we Vanesa ni Mpare wewe asa kiingereza cha nini.