Gebo tutaendelea kukumbuka

Wadau kadhaa wa soka walijitokeza

Maandalizi ya Michango ikiendelea

Msemaji wa familia ya Marehemu Gebo Peter, Peter Tino ambae pia ni kaka wa marehemu (wa kwanza aliesimama) akiwa pamoja na baadhi ya wachezaji wa zamani kulia kwake ni Aboubakar Kombo aliekaa kuanzia kulia ni Idi Pazi ambae ni kocha wa makipa wa Simba akifuatiwa na Khamis Kondo na David Mwakalebela wakiwa nyumbani kwa marehemu Vingunguti 


MCHEZAJI wa zamani wa timu ya  Gebo Peter (53)amefariki dunia juzi katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa siku moja.

Mchezaji huyo wa zamani alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya henya pamoja na kiuno ambapo alianzia kulazwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa siku tatu.


Kwa mujibu wa msemaji wa familia ya marehemu ambae pia ni kaka wa Gebo Peter, Peter Tino alisema kuwa marehemu wakati akiwa amelazwa katika hospitali ya Mwananyamala alizidiwa na ndipo wakampelekea Muhimbili alipolazwa kwa siku moja.


Tino alisema kuwa Gebo anatarajiwa kusafirishwa kwenda kuzikwa Kigurunyembe mkoani Morogoro leo ambapo saa tatu asubuhi wataanza kuaga mwili.


Alisema kuwa marehemu ameacha mke na watoto wa tatu ambao ni Lily,Elizabeth na Gregory.


"Kesho kuanzia saa tatu zitaanza shughuli za kumwaga na watu wanaotaka kuja kumwaga wanaweza kufika hapa nyumbani kwake Vingunguti karibia na Kanisa la Roman Catholic na kisha kwenda Kigurunyembe kwa maziko mkoani Morogoro"alisema Gebo Peter.


Nyumbani kwa marehemu walikuwapo wachezaji mbalimbali  wa zamani wa Yanga, Simba na timu nyingine mbalimbali za zamani ambao kila mmoja aliongelea namna alivyokuwa akimfahamu marehemu.

Related

Yani nina watoto kisha huyu tumbili ananitukana!!! Werema

Na Mwandishi Wetu, DodomaTAFRANI iliyojitokeza bungeni juzi kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema kumuita Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR Mageuzi) tumbili, naye kumjibu ...

The Voice --tunaifikia jamii kwa nyimbo za Injili

Kundi la Muziki wa Gospel la The Voice limesema kuwa litaendelea kutoa elimu zaidi ya Mungu kwa njia ya muziki. Kundi hilo mwaka huu linatimiza miaka 20 tangia kuanzishwa kwake. Kundi hilo linalou...

Bang Magazine yagonga miaka 10, yafanya sherehe, The Voice yaburudisha vema

Elgiver alifungua mvinyo The Voice waliwakilisha Mwanamuziki Yvone Sangudi ambae ni Mtanzania anaefanya shughuli zake za muziki Marekani alikuwapo Mtoto anaimba huyu Emelda Mkurugenzi ...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

item