Waziri wa Afya afungua wa Kongamano la 23 la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa mwaka wa wanachama Chama Cha Madaktari Bingwa wa Uzazi na Magonjwa ya Wanawake Tanzania (AGOTA).

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Seif Rashid (kushoto) Rais wa Agota wa Agota, Projestine Muganyizi pamoja na
daktari bingwa wa magonjwa ya  Bingwa wa Uzazi na Magonjwa ya Wanawake
Waziri akihutubia

Picha ya pamoja




Waziri akiondoka

Waliohudhuria

Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewataka madaktari Bingwa wa Uzazi na Magonjwa ya Wanawake kutokata tamaa katika kuwahudumia wajawazito nchini.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Seif Rashid katika uzinduzi wa Kongamano la 23 la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa mwaka wa wanachama Chama Cha Madaktari Bingwa wa Uzazi na Magonjwa ya Wanawake Tanzania (AGOTA).

 Kongamano hilo la siku tatu lilianza juzi na linamalizika leo, Dar es salaam  ambapo Pinda alisema kuwa serikali itaendelea na juhudi za kusaidia chama hicho.

Katika hotuba yake hiyo Pinda alisema kuwa anatambua uhaba uliopo wa asilimia 50 kwenye kada ya udaktari ambao unapelekea daktari mmoja kuwajibika kuwahudumia watu 39,000 na hivyo kuwa na athari kubwa zaidi kwa wajawazito na watoto wachanga.

Alisema kuwa kwa sasa takwimu bado zinaonesha kuwa vifo vya wajawazito na watoto wachanga bado vipo juu na lengo la kupunguza kiwango cha vifi halijafikiwa.

Alisema kuwa Malengo ya Milenia ambayo Tanzania ilijiwekea ni kupunguza kwa asilimia 75 vifo vitokanavyo na ujauzito pamoja na uzazi kutoka vifo 578 kwa kila vizazi 100,000 kufikia vifo 193 kwa vizazi hivyohivyo 100,000 ikifikapo mwaka 2015.

Aliendelea kusema kuwa hata kwa upande wa vifo vya watoto wachanga bado ni tatizo kwa kuwa kwa sasa takwimu zinaonesha kuwa vifo vimefikia 26 kwa uzazi 1,000 kinyume na lengo la Milenia la vifo 19 kwa vizazi 1,000.

Aliwataka madaktari kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Huduma Bora za Afya ya uzazi, wajawazito na watoto wachanga kwa wote ili kuhakikisha kuwa tatizo hilo linamalizwa.

Kwa upande wake Rais wa Agota, Projestine Muganyizi alisema kuwa mkutano huo ni wa siku tatu ambao ulianza juzi na unatarajiwa kumalizika leo.

Ni mkutano uliowashirikisha Madaktari Bingwa wa Mgonjwa ya Wanawake na Uzazi, Wanachama wa Agota pamoja na wanafunzi wa fani ya udaktari wote wakiwa wa kutoka mikoani na hapa Dar es salaam.

Related

Sticky 4369522361380112722

Post a Comment

emo-but-icon

item