Hebu yafahamu matokeo ya mwaka huu ya Form six
https://habari5.blogspot.com/2014/07/hebu-yafahamu-matokeo-ya-mwaka-huu-ya.html
BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA), imetangaza matokeo ya Kidato cha Sita uliofanyika kati ya Mei 5 hadi 21, 2014 ufaulu umeongezeka kwa asilimia 8.13 ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.
Kwa mwaka huu, wanafunzi 38,905 kati watahiniwa 40,695 ikiwa ni asilimia 95.98. Mwaka jana wanafunzi waliofaulu walikuwa ni 44,366 sawa na asilimia 87.85.
Kaimu Katibu Mkuu wa NECTA, Dk Charles Msonde alisema wanafunzi waliofaulu wasichana ni 12,080 sawa na asilimia 97.66 wakati wavulana ni 26,825 sawa na asilimia 95.25.
Alisema watahiniwa wa shule walioaulu ni wanafunzi 34,645 sawa na asilimia 98.26 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa ni 10,900 ambayo ni asilimia 99.2 na wavulana 23,45 sawa na asilimia 97.84. Mwaka 2013 watahiniwa 40,242 sawa a asilimia 93.92 ya watahiniwa wa shule waliauu mtihani huo.
" Mtahiniwa atahesabiwa kuwa amefaulu somo endapo atakuwa amepata angalau gredi D (alama 30) katika somo husika. Hivyo, kiwango cha juu cha ufaulu katika somo ni Gredi A ambapo kiwango cha chini cha ufaulu (pass) katika somo ni Gredi D. Ufaulu katika gredi A, B+, B na C utakuwa ni ‘Principal Pass’"
" Daraja la Kwanza limepangwa kwa poiti 3-7, la Pili 8-9, TAtu 10-13 na Daraja la Nne mtahiniwa watakuwa wamaaulu kwa kuwa na angalau D mbili au principal pass moja na aliyepata DAraja Siuri ni yule aliyepata ufaulu chini ya D mbili." alisema. Uzito wa alama katika Gredi; A=1, B+= 2, B=3, C=4, D=5, E=6 na F=7.
Alisema watahiniwa wa Kujitegemea waliofaulu ni 4,260 sawa na asilimia 80.73. ya watahiniwa 5,27 waliofanya mtihani. Mwaka 2013 Watahiniwa wa Kujitegemea 4,124 sawa na asilimia 53.87 walifaulu mtihani huo.
Msonde alisema Baraza limezuia matokeo ya watahiniwa 150 wa shule ambao hawajalipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa, watahiniwa tisa waliopata matatizo ya kiafya.
"Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya mtihani kwa masomo ambayo hawakuyafanya kwa sababu ya ugonjwa katika Mtihani wa Kidato cha Sita Mei, 2015.
Alisema watahiniwa 29 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa masomo yote. Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita Mei, 2015.
Msonde alisema Baraza limefuta matokeo yote ya watahiniwa wawili waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani.
Ubora wa ufaulu
Msonde alisema ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata Watahiniwa wa Shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 30,225 sawa na asilimia 85.73 wamefaulu katika madaraja I - III wakiwemo wasichana 9,954 sawa na asilimia 90.59 na wavulana 20,271 sawa na asilimia 83.53.
Daraja kwa Kwanza ni wanafunzi 3,773, wavulana 2,232 na wasichana 1,541, Daraja la Pili ni wanafunzi 9,631ikiwa wavulana ni 6,179 na wasichana 3,452.
Daraja la Tatu ni wanafunzi 16,821 ikiwa wavuana ni 11,860 na wasichana 4,961, Daraja la IV: wanafunzi 4,420 ikiwa ni wavulana 3,474 na wachana 946 na Daraja 0: wanafunzi 612, wavulana wakiwa ni 524 na wasichana 88.
Ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule
Msonde alisema ufaulu wa watahiniwa wa shule katika masomo yote (14) ya msingi umepanda ikilinganishwa na mwaka 2013. Ufaulu wa juu kabisa ni ule wa somo la Kiswahili ambao ni asilimia 99.88 ya watahiniwa wote wa Shule waliofanya somo hilo wamefaulu.
Alisema ufaulu katika masomo ya Sayansi (Physics, Chemistry, Biology na Advanced Mathematics) umeendelea kuimarika kwa kulinganisha na ufaulu wa masomo hayo mwaka 2013.
Shule zilizfanya vizuri
Msonde alisema wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha Wastani wa Pointi (Grade Point Average – GPA) na mchanganuo wa upangaji wa shule zilizofanya vizuri umezingatia shule zenye idadi ya watahiniwa wasiopungua 30.
Alitaja shule hizo kuwa ni Igowole(Iringa), Feza Boys(Dar), Kisimiri (Arusha), Iwawa (Njombe), Kibaha(Pwani), Marian Girls(Pwani) Nangwa(Manyara), Utawa(Mbeya), Kibondo(Kigoma) na Kawawa (Iringa).
Shule kumi za mwisho
Msonde alizitaja shule hizo kuwa ni Ben Bella( Unguja), Fidel Castro(Pemba), Tambaza(Dar), Muheza High School(Tanga), Mazizini(Unguja), Mtwara Technical(Mtwara), Iyunga Technical(Mbeya), AL-Falaah Muslim(Unguja), Kaliua (Tabora) na Osward Mang'ombe( Mara).
Watahiniwa walioanya vizuri
Msonde alisema watahiniwa waliofanya vizuri zaidi wamepatikana kwa kuangalia wastani wa Pointi (GPA) kwenye masomo ya tahasusi pamoja na wastani wa alama za jumla walizopata.
Alitaja majina ya wanafunzi hao ni Isaack Shayo (St. Joseph Cathedral), Doris Atieno Noah(Marian Girls), Innocent Sabbas Yusufu(Feza Boys'), Placid Ezekiel Pius(Moshi), Benni Shayo(Ilboru), Abubakar Juma(Mzumbe), Mwaminimungu Christopher(Tabora Boys), Chigulu Japhaly(Mzumbe), Hussein Parpia (AL-Muntazir Islamic Seminary) na Ramadhani Ally Msangi(Feza Boys).
Watahiniwa kumi bora kwa masomo ya biashara ni Jovina Leonidas(Nganza), Nestory Makendi (Kibaha), Imma Anyandwile(Umbwe), Thersia Marwa na Grace Chelele(Loyola), Betria Rugila(Baobab), Jaqueline Kalinga(Weruweru), Tajiel Kitojo( Arusha), Shiriya Ramaiya(Shaaban Robert) na Mwanaid Mwazema(Weruweru)
Watahiniwa kumi bora wa masomo ya Lugha na Sanaa ni Lisa Mimbi(St. Mary Goreti), Rosalyna Tandau( Marian Girls), Joseph Ngobya(St. Joseph Cathedral), Aneth Mtenga na Idda Lawenja( Marian Girls), Edna Mwankenja( Kisimiri), Catherine Kiiza( St. Mary Mazinde Juu), Nancy Adonswai(Mwika), Mohamed Salmin(Mwanza) na Idrisa Hamisi( Mwembetogwa).