Jide amshirikisha Uhuru katika ngoma hii

MWANAMUZIKI wa muziki Bongo Fleva, Judith Wambura, Lady Jaydee ameachia wimbo wake mpya akimshirikisha mwanamuziki Uhuru wa Afrika Kusini.

Wimbo huo unaitwa Give Me Love ambao una maadhi ya blues huku ujumbe wake mkubwa ukiwa unahusiana na masuala ya mapenzi.

Akizungumzia wimbo huo, Lady Jaydee alisema kuwa ni wimbo ambao unalenga kumtangaza zaidi katika anga la muziki bara Afrika hasa akiwa kama mwanamuziki kutoka Afrika Mashariki.

Alisema kuwa ametumia muda mwingi kuanzia kuuandaa wimbo huo hadi kufikia hatua ya kurekodi na kuuimba.


"Mimi bado ninaendelea na harakati zangu za kulitafuta soko la dunia kwa kuwa ninaamini kuwa nina kipaji kikubwa cha kuweza kufanya hivyo na kwa hiyo nimeamua kuanza kwa kuimba na Uhuru mwanamuziki ambae anafahamika kwa uwezo wake"alisema Lady Jaydee.

Aliongeza kuwa " Huu ni wimbo ambao ninamini kuwa utafanya vema katika soko la muziki hapa nchini kwa kuwa umeandaliwa vema kuanzia kuimbwa hadi kurekodi kwake".

Kuhusiana na suala zima la Video ya wimbo huo, Lady Jaydee alisema kuwa inatarajiwa kuingia sokoni mwezi ujao kwa kuwa kwa sasa bado haijakamilika.

Alisema kuwa inaandaliwa nchini Afrika Kusini na inatarajiwa kuwa video yenye hadhi ya kimataifa.

Ni wimbo ulioandaliwa na mtayarishaji mahiri wa muziki nchini Afrika Kusini Dj Maphorisa.

Lady Jayde ni moja kati ya wanamuziki wakongwe hapa nchini ambao wamechangia maendeleo ya muziki wa Bongo Fleva huku kwa sasa akiwa anamiliki bendi yake pa moja na mgahawa wa chakula na kipindi cha Luninga.
===================

Related

Party ya uzinduzi wa filamu ya James Bond, Spectre

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE MicrosoftInternetExplorer4 ...

Deo wa Nirvana awafunza mamodo wa Black Fox

Kijana akionesha manjonjo yake kwa wataalamu wa fani hiyo Huyu alionesha uwezo wake wa kuimba ikiwa ni moja kati ya vipaji vinavyotakufutwa na Black Fox Models Ak katikati ambae yeye ku...

Star Times yaahidi makubwa zaidi

Meneja wa Operesheni wa king'amuzi cha Star Time Gaspa Ngowi kulia akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana huduma za king'amuzi hicho ikiwa ni sehemu ya huduma kwa wateja wa king'amuzi hicho ...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

item