Hebu pata kuyasikia haya kutoka kwa kundi la Tamthilia la Mahusiano


Wasanii wa kundi la Mahusiano wakiwa pamoja na Wadau wa sanaa

Hii ni picha kutoka maktaba ya blog hii

Mwijaku katika mchezo huo huwa anaigiza kama mwanaume ambae yupo makini sana na marafiki wa mkewe huku akiwahusisha na tuhuma za kuwa wanamtafutia mkewe huyo wanaume, sasa hapa inaonekana ni kama anammaindi huyo mwanadada pembeni ya mkewe, ni kama igizo fulani hivi.  


Na Mwandishi wa Blog hii
KUNDI la Mahusiano ni moja kati ya makundi yanayokuja kwa kasi kubwa hapa nchini katika tasnia ya maigizo.

Mchezo wa kundi hilo unarushwa katika kituo cha Luninga cha Clouds Tv ni moja kati ya michezo ya Luninga inayotazamwa zaidi kwa sasa.


Ni mchezo unaozungumzia maisha ya kila siku katika mahusiano yawe ya ndoa au mahusiano ya wapenzi wa kawaida.


Akizungumza na safu hii msemaji wa kundi hilo, Rachel Kuyunga ambae anaigiza kama mke wa Mwinjaku katika mchezo huo alisema kuwa lengo la mchezo huo ni kuonesha yake yanayotokea katika jamii.


Alisema kuwa katika jamii ya sasa kuna wanawake wengi wanakumbwa na kero mbalimbali katika mahusiano yao na wanashindwa kujua namna bora ya kukabiliana nayo na ndio mcheozhuo unatoa suluhu ya hayo yote.


Alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa ujumbe mzima unawafikia wananchi wamejipanga kuhakikisha kuwa wanafanya maonesho ya jukwaani.


"Kwa sasa tunaendelea na kuelimisha jamii kupitia maigizo hayo yanayooneshwa kwenye Luninga ila kwa muda ukifika tutaingia kwenye live Performance na hapo ndipo pia utakuwa mwanya wa kuonesha ukali wetu zaidi"alisema Rachel.


Wasanii wengine wanaotamba katika igizo hilo ni Aika Steven, Charles Mwendo, Davis Ng'indu, Mariam Rashid, Mwemba Burton, Neema Mbuya na Farida.

Related

Sticky 2399511972108727965

Post a Comment

emo-but-icon

item