Timua timua Fulham

TIMU ya Fulham umethibitisha kuondoka kwa viongozi wake wa benchi la ufundi ambao ni Rene Meulensteen, Alan Curbishley na Ray Wilkins.

Uwepo wa wataalamu hao katika timu hiyo  ulionekana kuwa hatarani tangia mwanzo baada ya kuchaguliwa kwa kocha mpya wa timu hiyo Felix Magath ijumaa iliyopita.

Meulensteen alikuwa kocha mkuu wa timu hiyo kabla ya kuwasili kwa kocha mpya Magath huku Curbishley na Wilkins wakikaimu nafasi ya ukurugenzi wa ufundi pamoja na ile ya kocha mkuu msaidizi.

Uongozi wa Fulham ulitangaza Jumanne iliyopita kuwa makocha hao watatu pamoja na watu wengine ambao ni Jonathan Hill na Mick Priest wameacha kazi klabuni hapo.

Huku nafasi za hao wawili wengine zikichuliwa na Tomas Oral pamoja na Werner Leuthard.
Mwenyekiti wa Fulham, Shahid Khan alisema kuwa amekuwa akifanya kazi kwa furaha na makocha na kuwatakia kila la heri wanakoenda kwa kuwa wanao uwezo mzuri kikazi.

Alisema kuwa kwa sasa timu inapambana kuhakikisha kuwa inasonga mbele na kuwa moja kati ya timu kubwa katika Ligi Kuu England.

Fulham kwa sasa ipo chini katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi nne na inakabiliwa na mchezo dhidi ya West Brom kesho.

Related

Sport 1154475363975290997

Post a Comment

emo-but-icon

item