Rooney aanza kukata tamaa

MSHAMBULIAJI wa timu ya Manchester United, Wayne Rooney ameanza kuonesha kukata tamaa ya timuyake kuchukua kombe la Ligi Kuu England.

Timu hiyo kwa sasa ina Points 16 huku ikiwa nafasi ya saba.


Rooney alisema kuwa anaona kwa sasa labda wajitaidi kuhakikisha kuwa wanamaliza ligi wakiwa angalau kwenye hatua ya nne bora.


Alisema kuwa wamekuwa mara kwa mara wakitaka kushinda kombe lakini inaonekana kuwa ni hatua ngumu na ambayo haitowezekana kabisa kwa sasa kwa klabu yao hiyo kuifikia.


Tangia kocha wa sasa Davies Moyes kuchukua madaraka kutoka kwa aliekuwa kocha wa timu hiyo Sir Alex Ferguson imepoteza mechi 8 kati ya 24.


Lakini hata hivyo Rooney amemsifia kocha huyo kuwa ni kocha mzuri na mwenye uwezo wa hali ya juu na alikuwa akimtambua tangia akiwa kocha katika klabu ya Everton wakati huo Rooney akiwa anachezea klabu ya watoto.


"Huyu ni kocha ambae nimemfahamu muda mrefu ni kocha mzuri na mwenye kujua anachokifanya na kwa sasa anatakiwa kuwa na wachezaji wazuri tu watakaomsaidia na ndio ambacho tunatakiwa kufanya"Alisema Rooney.


Rooney ambae mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu ujao hakuwa tayari kuzungumzia hatma yake ya kuendelea kuitumikia klabu yake hiyo ya Manchester au ndio atahama.

Related

Kidume chenye mvuto Marekani

Jaji wa shindano la kuimba ya NBC singing show juzi alitajwa kuwa ni mwanaume mwenye mvuto zaidi kupitia jarida la People Magazine. Jamaa huyo ni mwanamuziki Adam Levine  ni kijana huyo wa m...

Namtambulisha kwenu msanii huyu anaitwa Kadija

MSANII Kadija ni moja kati ya wasanii ambao wameanza kusikika hivi karibuni katika medani ya muziki hapa nchini. Ni msanii ambae kwa sasa wimbo wake wa Maumivu ndio unatamba ...

Pata different pictures and habari kamaili kutoka Lake Oil India Food Festival

Esi na mwanawe Wadau mbalimbali waliokuwapo Mustapha na wageni Kids playing Imx na Mercy Imx na Mercy with friends Familia nyingi zilijitokeza Sarah akiwa na watoto ...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

item