Wekeni mbali nyimbo zangu na wanafunzi = Lil Wayne


MWANAMUZIKI machachari wa Marekani Lil Wayne, amewataka walimu wa ngazi mbalimbali za elimu kuacha kutumia mistari ya nyimbo zake kuwafundisha wanafunzi.

Rapper huyo alisema kuwa hakuna haja ya kutumia maneno wala misemo mbalimbali aliyokuwa akiitumia kwenye  nyimbo zake kama njia za kuwafundishi wanafunzi.


Hiyo imekuja kufuatia mwalimu mmoja wa shule ya awali iliyopo Kusini mwa Frolida, The Charter School of Boynton Beach kusimamishwa kazi mwezi huu kufuatia kuwapatia home work wanafunzi inayohusiana na nyimbo za msanii huyo.


Lil Wayne alisema kuwa akiwa anarekodi nyimbo zake hizo ana imani anawakilisha ujumbe mzuri na wenye kulenga kuleta mabadilio kwa wanajamii.


Lakini hata hivyo aliongeza kuwa nyimbo hizo zinaweza zikawa hazina ujumbe mzuri kwa watoto kwa kuwa mara zote zinalenga kuwazungumzia watu wazima na kubadilisha matukio mbalimbali ya watu hao.


Alikuwa akihiojiwa na jarida la ESPN alijitetea kwa kuwa sema kuwa haijawahi kutokea akatunga wimbo na kusema kuwa huu ni wimbo wa watoto ila anatunga nyimbo akilenga ujumbe kufika kwa wanajamii na sia lazima watoto wafundishwe.


"Mimi nikitunga nyimbo zangu huwa kwanza silengi na wala sipendi watoto wasikie na kama wakisikia ndio basi tena wanakuwa wameshasikia lakini sio lengo langu"alisema mwanamuziki huyo.


Aliongeza kuwa"sasa wewe kama mwalimu au mlezi ukiwalazimisha wanafunzi kusikiliza na tena kuwapatia home work kulingana na ujumbe kwenye nyimbo zangu unakuwa umewakosea watoto hao"


Mwalimu huyo wa kiingereza aliwaandikia wanafunzi home work kutokana na wimbo wa Lil Wayne uitwao Six Foot Seven Foot na kutaka waelezee maana yake ni nini katika jamii.
=================================

Related

Sticky 2271517096608229673

Post a Comment

emo-but-icon

item