Baiskeli 317 zatolewa kwa wanafunzi wanaoishi mbali na shule
https://habari5.blogspot.com/2014/03/baiskeli-317-zatolewa-kwa-wanafunzi.html
Na Mdau wa elimu
MKAKATI wa kujenga uwezo kwa shule za sekondari unaosimamiwa na Uholanzi kwa kushirikiana na Taasis ya Elimu nchini (TET) imekabidhi jumla ya baiskeli 317 ili kuwasaidia usafiri wanafunzi wanaoishi mbali na shule.
Baiskeli hizo zitatumika kwa shule za msingi na sekondari za Dar es Salaam na Pwani.
Makabidhiano ya baiskeli hizo yalifanyika jana Dar e s Salaam na Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Eustella Bhalalusesa ambae naye alizikabidhi kwa baaadhi ya wanafunzi wenye matatizo ya usafiri.
Akizungumza, Kamishana Eustella alisema ubora wa elimu unategemea mafanikio ya walimu pamoja na ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali.
Aidha aliwataka wadau wa elimu kuzingatia kusaidia walimu kwani wengi wao huishi katika mazingira magumu na mbali na shule wanazofundisha.
Alisema walimu pamoja na wanafunzi wanajukumu kubwa katika kufikia mafanikio ya elimu kwani mmoja hawezi kuwa peke yake bila mwingine hivyo wadau wa elimu wasielekeze nguvu zao kwa wanafunzi pekee, waangalie pia kwa waalimu.
Alisema shida ya usafiri ni tatizo kubwa linalowakabiliwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika mikoa husika hususani nyakati za asubuhi na jioni ambapo hukumbana na matatizo mbalimbali kutoka kwa makondakta yanayowasababishia kuchelewa kufika shuleni.
Awali akizungumza, Kaimu Mkurugenzi wa TET Dr Leonard Akwilapo alisema wanafunzi walio wengi hukumbana na shida ya usafiri ambayo huwasababishia athari katika masomo yao.
“Katika mipangilio ya shughuli za kila siku, ushirikiano na wanafunzi ni jambomuhimu, ndani ya miaka miwili tumekuwa wamoja ili kupata mrejesho wa utekelezaji wa mitaaala,” alisema Akwilapo.
Alisema kwa ushirikiano huo, TET imeweza kubaini matatizo yanayoikabili ufundishaji haswa suala la usafiri ambapo kumewezesha taasisi hiyo ya Uholanzi kutupatia baiskeli hizo ambapo pia taasisi hizo zimeanda kozi ambazo zitakuwa zikifundishwa kwa wanafunzi katika jiji la Dar e s Salaam.
mwisho