Said Fella akerwa na mameneja wanyanyasaji

MENEJA wa kundi la TMK Wanaume Family Said Fella amewataka mameneja wa muziki nchini kutambua kuwa kuwa meneja wa msanii ni kazi kama kazi nyingine.

Fella ambae ameliongoza kundi la TMK Wanaume Family kwa muda mrefu huku likiwa ni kundi ambalo linazidi kumarika kila kukicha.


Fella aliiambia safu hii kuwa wapo mameneja ambao wanafanya kazi vema zaidi na wasanii wao kwa kujua kila kile kinachotakiwa kufanyika huku kukiwa na mameneja ambao wanawadharirisha wasanii.


Fella aliiambia safu hii kuwa amekasirishwa na kujisikia kufedheheshwa na namna ambavyo meneja wa kundi la Mtanashati aitwae Ustaadhi Juma kwa kitendo chake cha kumfedhehesha alikuwa msanii wake PNC.


Alisema kuwa meneja huyo kitendo cha kupigiwa magoti na msanii huyo akiombwa msamaha na kisha akaiweka picha hiyo kwenye mtandao wa kijamii ni kitendo kibaya .


"Tusiwe Mungu watu sisi mameneja kwa wasanii wetu, ila tunachotakiwa kujua kwa sasa kuwa tunafanya kazi na wasanii ambao haohao ndio mabosi wetu sasa tukichefuana tuelewane kiustaarabu na sio vinginevyo"alisema Fella.

Related

Sticky 7732236155708084714

Post a Comment

emo-but-icon

item