Tressa sasa inapatikana nchi nzima angalia ilivyozinduliwa Mwanza
https://habari5.blogspot.com/2014/03/tressa-sasa-inapatikana-nchi-nzima.html
live workshop on Tressa Prodcuts during its launch in Mwanza on 24 March 2014 |
invited guest dancing to SHAA music during Tressa Mwanza Launch |
Mayor Mabula Apprciating Tressa Products - |
Mayor of Mwanza Stanley Mabula with Saloon Owner Flora Lauwo |
The Mayor awarding a lucky winner a gift hamper |
Singer Vanessa Mdee Performing at Launch of Tressa in mwanza |
prolific performing artiste SHAA performing during the Tressa Lauinch in Mwanza on 24 March 2014 |
various invited Saloon owners at Tressa Launch in Mwanza |
Hatimaye bidhaa ya vipodozi vya nyewele ya Kitanzania ijulikanayo kama TreSSa Proffesionals imezinduliwa leo katika hoteli ya Golden Crest ,jijini Mwanza. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wamiliki wa saluni, wanamuziki na wanamitindo maarufu na waandishi wa habari. TreSSa Proffesionals ni bidhaa mpya ya vipodozi vya nyewele iliotengenezwa mahususi kwa ajili ya nywele za mwanamke wa Kitanzania.
Tressa Professionals ni ubunifu kwenye tasnia ya utunzaji nywele, ikiwa na mchanganyiko wa kipekee wa sayansi na asili. Bidhaa za TreSSa zina viungo kama vile; Parachichi, Mafuta ya Jojoba, Indian Hemp na protini za nywele kama vile Keratin.
Bidhaa hizi vimefanyiwa uchunguzi na kujaribiwa kwenye nywele za Kitanzania na kumpa Uhuru mwanamke wa Kiafrika wa kutokatika kwa nywele. Sasa mwanamke ana uhuru wa kuchagua bidhaa inayoendana na mtindo wa nywele aupendao.
TreSSa ina bidhaa mbalimbali za vipodozi vya nywele zikiwemo; Relaxers (aina ya regular na super), Neutralising plus Strengthening Shampoo inayoweza kutumika kila siku, Hair Food (iliyo na mafuta ya Jojoba na Indian Hemp) inayong’arisha na kupoza nyewele na ngozi ya kichwa, Moisturising Pink Lotion kwa matumizi ya kila siku na Hair Mayonnaise iliyo na protini kwa nywele zenye afya.
Akiongea na waandishi wa habari, Afisa Mkuu was masoko , Chemi cotex, Bwana R.N. Ojha, alisema, “Kampuni ya Chemicotex imekuwa mstari wa mbele kuleta bidhaa zenye ubora kwa watu wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. TreSSa ni mfano wa ahadi endelevu wa ahadi zetu wa kutoa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kwa watu wa Tanzania”.
Tressa Professionals ni bidhaa iliyotengenezwa na kampuni ya Chemicotex, ambao ni watengenezaji maarufu wa dawa ya meno ya Whitedent na Bannister’s Glycerine.
Afisa Meneja wa kitaifa was biashara wa masoko, Chemicotex, Bwana Manoj Kumar, alisisitiza, “Utafiti umetuonyesha kwamba utunzaji wa nywele ni jambo la muhimu kwa wanawake wa Kitanzania. Hatimaye TreSSa imewapa wanawake uhuru wa kutokatika kwa nywele, ambalo ni tatizo kwa wanawake wengi wakati wakitengeneza nywele.”
Tuna mipango ya kuwafikia wanawake wote nchini kupitia semina, warsha, vipindi vya tv na ushirikiano wetu na saluni ili kuhakikisha mwanamke anapata fursa ya kutengeneza mitindo ya nywele aipendayo kwa kutumia TreSSa.” Bwana Ojha aliongezea alipokuwa akizungumzia mipango ya TreSSa.
Kampuni hii ina mipango madhubuti ya kimasoko na kuitangaza bidhaa ya TreSSa, aidha kampuni ina malengo ya kumiliki asilimia 25 ya soko la utunzaji nywele ndani ya miaka 3.