MAJINA ya washiriki wa shindano la Tuzo za Muziki za Kilimanjaro yalitangazwa jana ambapo msanii Nasib Abdul, Diamond, pamoja na Judith Wambura, Lady Jaydee wanaumana katika vipengele viwili.
Pia nyimbo za wasanii Uzuri Wako ulioimbwa na Jux, Nimevurugwa wa Snura na Tema Mate Tuwachape wa Madee zimeondolewa kwenye shindano hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mwingereza alisema kuwa shindano hilo linashirikisha vipengele 32.
Alisema kuwa jumla ya kura zilizopigwa ni elfu 30 kuchagua wasanii wa kuingia kwenye vipengele mbalimbali.
Aliongeza kuwa upigaji rasmi wa kura kuwapigia washiriki ni April mosi mwaka huu hadi April 31 na majina ya washindi kutangazwa katika vyombo vya habari.
Aliongeza kuwa hafla ya utoaji wa tuzo hiyo itafanyika Mei 3 mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City.
"Mambo ndio yameanza kuiva katika tuzo za Kili mwaka huu na kuna mabadiliko ambayo tumeyafanya kama Basata ambapo kuna wasanii tuliowatoa kutokana na nyimbo zao kutokuwa na maadili katika Video zao"alisema Mwingereza.
Katika vipengele 32 vinavyoshindaniwa katika tuzo hizo msanii Diamond na Lady Jaydee wanaumana katika kipengele cha wimbo bora wa mwaka.
Diamond anashindana kupitia wimbo wake wa Number One, huku Lady Jayde akiwa na nyimbo mbili ambazo ni Joto Hasira na Yahaya.
Wengine kwenye kipengele hicho ni pamoja na wimbo wa I Love You wa Cassim Mganga, Kidela wa Abdul Kiba na Muziki Gani wa Ney wa Mitego.
Lady Jaydee anakuja kukutana tena na Diamond kwenye kipengele cha wimbo bora wa Afro Pop. Katika kipengele hicho Diamond anashindanisha tena wimbo wake ule ule wa Number One huku safari hii Lady Jayee anashindanisha wimbo wake wa Joto Hasira.
Rich Mavoko kupitia wimbo wake wa Roho Yangu, Ommy Dimpoz kupitia wimbo wake wa Tupogo,Abdul Kiba anaingia tena kupitia wimbo wake wa Kidela.
Baadhi ya vipengele vingine vinavyoshindanishwa ni pamoja na Wimbo bora wa Raggae,Afro Po,Raga na Dancehall,Taarab, R and B,Zoukd Rhumba, Afrika Mashariki na Hip Hop.
Pia kuna vipengele vya msanii bora wa kiume wa muziki wa kizazi kipya, taarab, mwimbaji bora wa kiume kutoka katika bendi, mwimbaji wa kike katika taarab, kizazi kipya na pia katika bendi. Wimbo bora wa kushirikiana, wimbo bora wa kiswahili.
Wasanii wengine wanaoshindana katika kipengele hicho ni pamoja na
|