Rick Ross ataja mambo usiyoyajua yanayomhusu

MSANII mahiri wa muziki wa kugani, Hip Hop  Rick Ross ametaja mambo mbalimbali ambayo anaona kuwa washabiki wake hawayajui.

Alisema kuwa anataka wapenzi wake wa muziki kujua mambo yote muhimu kuhusiana na kazi zake za sanaa, maisha yake binafsi pamoja na mengi kuhusiana na yeye.


Alisema kuwa kwanza anapenda sana kutumia michezo ya Video Games ambapo anamiliki baadhi ya michezo yake mwenyewe.


Alisema kuwa kitu kingine ni hupenda kucheza video game kabla ya kuanza kurekodi nyimbo zake kwa kuwa anaamini kuwa kwakufanya hivyo inasaidia kupunguza mawazo.


Alitaka kitu kingine ni kwamba analala saa mbili hadi tatu kwa usikum, na kuongeza kuwa ana tatoo zaidi ya 500 mwilini mwake.


Aliongeza kuwa kitu kingine ambacho alitaka wapenzi wake wajue ni kwamba alichora tatoo yake ya kwanza akiwa na miaka mitatu.


Alisema kuwa alikuwa akicheza mpira katika shule ya Miami Carol City Senior High School wakati akisoma sekondari na aliongeza kuwa wakati wa mapumziko alikuwa akiendelea na masuala yake binafsi mbali na mpira.


Aliongeza kuwa kila siku usiku ni lazima apige magoti kusali kumuomba Mungu abariki shughuli zake za muziki.


Alisema kuwa jina la Rick Rose lilitokana na jina la Rick Rozay kutokana na kupenda kunywa wine na kuongeza kuwa anapenda kunywa kinywaji cha wine aina ya Belaire Rose.

Related

Sticky 7015147527811333144

Post a Comment

emo-but-icon

item