Kanye West na Kim wapata upinzani
https://habari5.blogspot.com/2014/03/kanye-west-na-kim-wapata-upinzani.html
|
JARIDA la maarufu nchini Marekani na dunia nzima kwa ujumla la Vogue limepingwa kwa kutumia picha ya kurasa wake wa mbele unaowaonesha wapenzi maarufu duniani Kanye West pamoja na Kim Kardashian.
Mmoja kati ya watu waliopinga ni mwigizaji wa muda mrefu wa filamu wa Sarah Michelle Gellar ambae amesema kuwa anafikiria kusitisha kununua jarida hilo.
Hiyo imekuja muda mfupi baada ya kuthibitika kuwa jarida hilo litakalotoka mwezi ujao katika picha ya kurasa wake wa mbele kutakuwa na picha za wapenzi hao.
Mwigizaji huyo aliandika kwenye kurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ujumbe uliokuwa ukisisitiza kuwa anafikiria kuachana na jarida hilo.
Pia alituma ujumbe mwengine uliokuwa ukiuliza iwapo kama kuna watu walikuwa wakitaka kuungana nae katika kupinga matumizi ya picha hiyo.
Kwa upande wake mhariri wa jarida hilo la Vogue Anna Wintour alitetea uamuzi wake wa kutumia picha za wapenzi hao kwa kusema kuwa kuwa hakukuwa na shinikizo katika kuamua picha ya kutumia kwenye kurasa wa mbele wa Jarida hilo.
Alisema kuwa picha hizo zinapendeza kwa kuwa Kanye na mpenzi wake huyo wote wamependeza wanafuraha na hakuna hata mmoja wao ambae anachukiza kuwapo katika jarida hilo.
"Wote ni maarufu wakati Kanye akiwa ni mwanamuziki mpenzi wake huyo ni mdau mkubwa wa Mitindo na mwenye kupendwa duniani kote sasa kwa nini wasitumike hawa"alihoji mhariri huyo.
|