Simba yapigwa faini

BODI  ya Ligi Kuu Tanzania  bara (TPLB) imeipiga faini  klabui ya Simba ya jumla ya sh. milioni moja  kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo vitendo vinavyoashiria ushirikina uwanjani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura alisema  Simba ilifanya vitendo hivyo katika mechi yake dhidi ya Mbeya City  ambapo imepigwa faini ya sh. 500,000.

Pia imepigwa faini  ya sh. 500,000 kwa makocha wake Logarusic, Selemani Matola na Idd Pazi kuingia uwanjani na kumzonga mwamuzi kwenye mechi hiyo.

Naye,  mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushangilia bao alilofunga kwenye mechi hiyo kwa kuonesha ishara ya matusi kwa kidole.

Wakati huo, Mbeya City imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa washabiki wake kuingia uwanjani kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa mjini Bukoba.

Wambura alisema  pia  klabu za Yanga na Coastal Union zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa washabiki wao kurusha chupa za maji uwanjani wakati timu hizo zilipopambana jijini Tanga.

Aidha, kiungo wa Mtibwa Sugar, Shabani Nditi amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumpiga mchezaji wa Simba, wakati Salvatory Ntebe pia wa Mtibwa Sugar amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtukana refa kwenye mechi dhidi ya Mbeya City.

Alisema adhabu nyingine ni  kwa mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Musa Mgosi ambaye amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kosa la kupiga uwanjani kwenye mechi dhidi ya Ashanti United ambapo vilevile atakosa mechi tatu za ligi.

Coastal Union imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa washabiki wake kumrushia chupa za maji kipa wa Mbeya City.

Nayo, JKT Ruvu imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi dhidi ya Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Related

Sticky 3350629537613536475

Post a Comment

emo-but-icon

item