Stamico yafagilia ulinzi wa JKT mgodini
https://habari5.blogspot.com/2014/03/stamico-yafagilia-ulinzi-wa-jkt-mgodini.html
SHIRIKA la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa, SUMA JKT, limepongezwa kwa juhudi zake katika kuhakikisha ulinzi unaimarika katika maeneo ya mgodi wa STAMIGOLD uliopo Biharamulo Kagera.
Mgodi huo kwa sasa umekabidhiwa kwa serikali ambapo unaendeshwa chini ya shirika la madini la STAMICO.
Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa STAMICO, Rumisha Kimambo katika kikao kilichojumuisha Bodi yake na uongozi wa mgodi wa huo kilichofanyika mgodini hapo hivi karibuni.
Mwenyekiti huyo ambae pia alipata fursa ya kutembelea eneo la westzone na mojamoja uliopo Mgodi huo alionesha kuridhishwa na mfumo wa mbinu shirikishi zinazotumiwa na mgodi huo katika kulinda mgodi bila ya kuharibu uhusiano kati ya mgodi huo na wananchi.
“Tumefurahishwa sana na kazi inayofanywa na SUMA JKT hapa STAMIGOLD kwani wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuondoa tatizo la wachimbaji haramu na wavamizi ndani ya mgodi.”
Alisema kuwa wachimbaji haramu wengi katika migodi ni tatizo na kunakuwa na njia mbadala katika kuwakabili kitu ambacho SUMA JKT imefanikiwa.
Shughuli za uchimbaji katika mgodi huo zinatarajiwa kuanza mwezi April mwaka huu baada ya kukamilika kwa barabara ya urefu wa takribani Kilometa 3.9 kutoka eneo la ofisi za Mgodi kuelekea kwenye maeneo ya uchimbaji
Mapema mwezi huu kampuni ya African Barrick Gold iliyokuwa ikimiliki mgodi wa TULAWAKA ilifanikiwa kuhamisha kibali na baadhi ya leseni za uchimbaji katika eneo la westzone na mojamoja kwa shirika la madini STAMICO hivyo kuwezesha shirika hilo kuwa katika nafasi nzuri ya kuendeleza sekta ya madini hapa nchini.
===========