AY ala mzinga, ajali ilitokea njia ya kwenda Oysterbay

Msanii Ambwene Yesaya amenusurika katika ajali ya gari iliyotokea hivi karibuni katika daraja la Surrender lakini hata hivyo hakuumia. Msanii huyo aliiambia blog hii kuwa alikuwa akitokea kumshusha mshkaji wake msanii kutokea nchini Kenya aliekuwa hapa nchini kwa shughuli binafsi.  


 Ay alisema kuwa ilikuwa majira ya saa tano usiku ambapo aliemgonga ndio mwenye kosa kwa kuwa alikuwa amepita kwenye njia panda huku taa zikiwa hazijamruhusu na kuongeza kuwa hata hivyo gari lake aina ya Prado limeharibika.

Alisema kuwa kwa sasa amesharipoti katika kituo cha Central na kesi inashughulikiwa.

Blog hii itakuwa ikiendelea kutoa updates mbalimbali kadiri tutakavyokuwa tukizipata

Related

Sticky 6344835317736375759

Post a Comment

emo-but-icon

item