Presidaa Nyoshi amkubali Menina
https://habari5.blogspot.com/2014/04/presidaa-nyoshi-amkubali-menina.html
Msanii wa muziki wa Bendi ya FM Academia ambae ni kiongozi wa bendi hiyo, Nyoshi El Sadaat ameonesha nia ya kufanya kazi na msanii anaechipukiza kwa kasi kwa sasa Menina.
Nyoshi alisikiwa na safu hii akimsifia msanii huyo na kusema kuwa angependa siku moja kufanya nae kazi.
Ilikuwa kwenye semina ya Tuzo za Kili kwa wasanii wa muziki ambapo Nyoshi alisema kuwa anampenda sana msanii huyo kutokana na uwezo wake wa kuimba kucheza na hata nidhamu yake ya kazi.
Alisikika akisema kuwa anahitaji siku kufanya nae kazi na tena alifikia hatua ya kuchukua namba yake ya simu.
"Yani wewe mtoto ni wa ukweli na unajua nini unachokifanya katika muziki, kwanza nashukuru katika semina hii tumekutana na tunazungumza pamoja na nina imani kuwa ipo siku hata kazi tutafanya pamoja"alisikika Nyoshi akimwambia msanii huyo.
Alisema kuwa amekuwa akifuatilia Video zake na kuwa ni msanii anaejua nini anachokifanya akiwa kazini.