Bongo5.com yaja na tuzo za watu
https://habari5.blogspot.com/2014/04/bongo5com-yaja-na-tuzo-za-watu.html
Nacy akizungumza na waandishi |
Miss Tanzania 2005 ambae pia ni Mkurugenzi wa Bongo 5 Media Group, Nancy Sumary akizungumza na Rama Nnauye. |
Mhariri Mkuu wa Bongo 5.com Tuzo hizo Fredrick Bundala na kushoto ni ofisa kutoka kampuni hiyo Rama Nnauye. |
WADAU na wasiokuwa wadau wa Sanaa, michezo pamoja na habari wametakiwa kuzitumia vema tuzo za watu zenye lengo la kutambua mchango wa wanamichezo, wasanii na watangazaji katika jamii ya kitanzania.
Katika tuzo hizo watu mbalimbali wanaruhusiwa kupiga kura kuchagua watu wanaowapenda kutwaa tuzo hizo ambazo upigaji wa kura huo umeanza tangia jana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Bongo5 Media Company, hiyo ambayo inamilika gazeti tando, blog maarufu ya sanaa na michezo ya Bongo 5, Nancy Sumari alisema kuwa kilele za tuzo hizo ni mwezi Juni.
Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kupendekeza majina ya watu wanaodhani kuwa wana mvuto katika sekta zilizotajwa.
"Upekee wa tuzo hizi ni kuwa majina yote ya washiriki watakaoshindanishwa kuwania tuzo, kuanzia mwanzo hadi mwisho yatachaguliwa na wananchi wenyewe na sio kundi la watu wachache kwenye tasnia husika"alisema Nancy.
Aliongeza kuwa "tuzo za watu zinalenga kuanzisha mchakato wa wazi na huru wa utambuzi wa watu wenye umuhimu na michango mahsusi katika nyanja mbalimbali,wanaochaguliwa moja kwa moja na wananchi wenyewe".
Tuzo hizi zitatumika kuanzisha urithi utakaoleta hatua mpya ya heshima kwenye jamii yetu.
Kwa upande wake Mhariri Mkuu wa Bongo 5 Blog Fredrick Bundala alisema kuwa awamu ya kwanza ya upigaji kura itakusanya kura kwa muda wa wiki mbili kutoka siku ya uzinduzi wa tuzo, na baadaye majina ya wanaowania tuzo watano, ambao wameongoza kwa kura zaidi, kutoka kwenye kila kipengele, wakitangazwa kuendelea kwenye mchakato wa kuwania tuzo.
"Kuanzia hapo na kuendelea, upigaji kura wa wananchi utajikita tu katika orodha ya majina hayo matano, yaliyotangazwa kuongoza kwa kura, kwenye kila kipengele alisem Bundara.
Alisema kuwa wiki moja baada ya majina ya washiriki watano kutangazwa, mchujo wa kwanza utafanyika katika kila kipengele na kati ya wanaowania,mmoja ataondolewa na kubakiza wanne.
Alisema kuwa wiki moja baada ya mchujo huo wa kwanza, mchujo wa pili utafanyika na kuwabakiza wanaowania watatu kwenye kila kipengele.
"Wanaowania tuzo wote (watatu katika kila kipengele) waliosalia baada ya kufanyika mchujo wa pili na (wa mwisho), watakuwa wageni wa heshima kwenye utoaji wa tuzo hizo, utakaofanyika wiki mbili baada ya mchujo huo wa pili, ili kutoa nafasi ya mashabiki wao kuendelea kupiga kura"aliongeza.
Alimalizia kuwa kkila mshindi atakayetangazwa, atapokea zawadi ya fedha taslimu, shilingi 1,000,000 za Kitanzania pamoja na tuzo ya thamani iliyotengenezwa kwa mkono kutoka kwenye mali ghafi za asili ya Kitanzania.