Coca Cola yazindua prmosheni ya kwenda Brazil




 Meneja wa Kinywaji cha Coca Cola Maurice Njowoka akizungumza na waandishi wa habari
Meneja Mkazi wa Coca Cola Yebeltal Getachew akisisitiza jambo


Picha ya Pomoja



 


Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Coca Cola jana ilizindua promosheni yake ya miezi miwili ambapo wateja wake watajishindia zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na tiketi ya kwenda Brazil kushuhudia mchezo wa robo fainali wa Kombe la Dunia.


Akizungumza na waandishi wa habari jana Meneja Mkazi wa Coca Cola Tanzania, Yebeltal Getachew alisema kuwa wateja 14 watashinda nafasi ya kwenda Brazil kushuhudia michuano hiyo.


Alisema kuwa katika promosheni hiyo pia luninga 1000 za kisasa aina ya sony LED zenye ukubwa wa inchi 32, pamoja na mipira 8,000 yenye nembo ya FIFA World Cup zitashindaniwa.


Aliongeza kuwa mbali na zawadi hizo pia kutakuwa na fulana 30,000 ambapo alisema kuwa wateja wengi wa kinywaji cha Coca Cola watanufaika na promosheni hiyo ya aina yake.


Alisema kuwa lengo la promosheni hiyo ni kuwaweka karibu zaidi wateja wa Coca Cola na fainali hizo za kombe la dunia ambazo zimekuwa zikidhaminiwa na kinywaji hicho kwa muda mrefu.


"Najua tangia miaka ya 1970 kinywaji hichi kimekuwa karibu na Kombe la Dunia ambapo wateja wake wamekuwa wakinufaika kwa namna mbalimbali hivyo basi kwa mwaka huu zawadi hizi ni muendelezo wa kuwaweka karibu zaidi watanzania na fainali hizo kupitia Coca Cola"alisema Getachew.


Pia katika kuongeza hamasa ya kombe la dunia kupitia kinywaji hicho  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Judith Wambura, Lady Jaydee ameshiriki katika wimbo wa kushabikia kombe hilo akiwa pamoja na msanii mwengine kutoka Kenya, Octopizo pamoja na msanii maarufu wa Marekani mwenye asili ya Brazil aitwae David.


Wimbo huo umeimbwa kwa kutumia lugha mbalimbali za mataifa mbalimbali na kwa ukanda wa Afrika Mashariki wameshirikishwa wasanii hao wakiwa na msanii huyo wa Marekani.
==============

Related

Sticky 5708699553883412168

Post a Comment

emo-but-icon

item