Sina mpango wa kuolewa tena === Kajala
https://habari5.blogspot.com/2014/04/sina-mpango-wa-kuolewa-tena-kajala.html
MSANII wa filamu nchini, Kajala Masanja amekanusha kuwa na uhusiano na wanaume na kusisitiza kuwa kwa sasa anaendelea kumsubiria mumewe alieko gerezani.
Kajala msanii ambae alianza kung'ara kupitia filamu ya Devil Kingdom aliposhirikishwa na marehemu Steven Kanumba na muda mfupi baadae alijikuta akiingia matatizoni kufuatia kushirikishwa kwenye uhalifu ambao unatuhumiwa kufanywa na mumewe.
Kajala aliiambia safu hii kuwa bado anampenda mumewe na anaendelea kumsubiria na hana mpango wa kuolewa na mwanaume mwengine kwa sasa.
Alisema kuwa akiwa kama muumini wa dini ya kikristu wa dhehebu la Roman Catholic hawezi kuolewa tena na kwa upande wake anaendelea kumsubiria mumewe huyo.
Lakini hata hivyo Kajala alitoa wito kwa wasichana kuwa makini kabla ya kuingia katika ndoa.
"Mimi niliolewa kwa kuwa nilikuwa na matatizo yangu mwenyewe na ndio maana nikaamua kuolewa lakini kumbe ndio nilijiingiza kwenye matatizo makubwa na kwa sasa naona kuwa ni bora ningetulia na kupenda kusoma"alisema Kajala.
Kajala hata hivyo alionesha kujuta kwa kutosikiliza ushauri wa wazazi wake waliokuwa wakimtaka kuendelea kusoma na yeye kujikuta akiendekeza masuala mengine ambayo hayana msingi kwake.
"Yani mimi kuna wakati najuta kwa nini sikuendelea na kusoma najua kuwa kwa sasa ningekuwa mbali na maisha yangu basi angalau yangekuwa na mwelekeo zaidi ya hapa natamani pengine hata ningekuwa nimeajiliwa sehemu saa hizi nakula mshahara wangu na kuwa na familia yangu"alisema Kajala.