NHIF watembelea ofisi za TSN na kuzungumzia uendeshaji wa mfuko wao huo

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NHIF, Hamisi Mdee akipokeza zawadi ya saa kutoka kwa Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya serikali ya TSN

Meneja wa uzalishaji TSN John Mcharo akizungumza na ugeni huo

Wakiendelea kupewa elimu

Kaimu Mhariri wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali, TSN Gabriel Nderumaki akizungumza na wageni kutoka NHIF waliofika ofisini kwake ikiwa ni sehemu ya ziara ya Mfuko huo kwa TSN

Picha ya pamoja

Mkuu wa uzalishaji Gkaro Sabai akiwaonesha wageni wa NHIF namna ambavyo gazeti linazalishwa

Mkurugenzi wa Masoko na Tafiti wa NHIF Raphael Mwamoto akifafanua jambo.
 Habari Kamili.

MFUKO wa Taifa wa Afya ya Jamii (NHIF) umewataka wananchi pamoja na wahudumu katika sekta ya afya kufichua wizi unaofanywa na waharifu wanaouza dawa nje ya utaratibu.

Wito huo ulitolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa NHIF, Hamisi Mdee wakati alipofanya ziara katika ofisi za kampuni ya magazeti ya serikali, TSN zilizopo Tazara.


Mdee ambae aliongozana na baadhi ya maofisa katika ziara yake hiyo ya kuimarisha mahusiano na vyombo vya habari alisema kuwa tatizo la ukosefu wa dawa katika hospitali nyingi linapaswa kutatuliwa kwa pamoja kwa ushirikiano wa NHIF, wananchi na wahudumu katika sekta ya afya.


Alisema kuwa NHIF kwa upande wake inajitaidi katika kuhakikisha kuwa kila hospitali inakuwa na dawa za kutosha na inafanya hivyo lakini changamoto kubwa inatoka kwa baadhi ya wauguzi wasiokuwa waadilifu.


Alisema kuwa baadhi yao wanauza dawa hizo katika vituo binafsi vya afya na hivyo kupelekea upungufu huo kujitokeza.


Aliongeza kuwa ili kukabiliana na hali hiyo inatakiwa ushirikiano kati ya wananchi kuwafichua wauzaji wanaofanya biashara hiyo katik ajamii zao na pia wahudumu wa afya kuwafichua wenzao wanaofanya uharifu huo.


"Hili ni suala ambalo linahitaji ushirikiano wa kila mtu na hasa katika kukabiliana na suala hili ili mwisho wa siku kila mtu anufaike na mfuko huu"alisema Mdee.


Aliongeza kuwa ili kuhakikisha kuwa NFIH inawafikia walengwa wake nchi nzima kwa sasa inakopesha Halmashauri ili kuhakikisha kuwa hospitali zake zinakuwa na dawa.


Aliongeza kuwa katika mpango huo Halmashauri zinachukua dawa kutoka Bohari Kuu ya Dawa au kwa wasambazaji binafsi na kisha wanapeleka madai yao kwa NHIF ambayo inawalipia dawa hizo.


Alisema kuwa mbali na juhudi kama hizo zifanywazo na Mfuko huo lakini mwisho wa siku inatakiwa kuwepo na usimamizi mzuri wa dawa hizo ili wanachama wanufaike.


Aliongeza kuwa kwa sasa NHIF ina wanachama asilimi 15 ya watu na ina mikakati ya kuhakikisha kuwa inaongeza idadi ya wanachama wake kufikia asilimilia 30 ifikapo mwakani.


Akizungumzia ziara hiyo Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Gabriel Nderumaki alisema kuwa ni ziara yenye kulenga kuimarisha uhusiano wa kitaasisi kati ya TSN na NHIF.


Alisema kuwa TSN kama kampuni kubwa ya magazeti ya serikali ina mengi ya kufanya kwa pamoja na NHIF ikiwa ni njia mojawapo ya kuimalisha maendeleo yake na pia kuwasaidia katika kutangaza kazi zao kwa manufaa ya jamii.


"Kuna mengi ya kiutendaji ambayo sisi kama TSN tunapaswa kufanya na NHIF lakini pia hapo hapo inatakiwa kuhakikisha kuwa tunawaelimisha wanajamii kupitia magazeti yetu mambo mengi kuhusiana na NFIH hasa hilo la wizi wa dawa ili mwisho wa siku jamii nzima inufaike na mfuko huu"alisema Nderumaki.
==============

Related

Sticky 7266566246650043706

Post a Comment

emo-but-icon

item