Proin Promotions yazidi kuchanja mbuga kusaka vipaji vya uigizaji
https://habari5.blogspot.com/2014/04/proin-promotions-yazidi-kuchanja-mbuga.html
CODES:
Anasema lengo la PPL kuzungukia kanda hizo sita nchini ni kuhakikisha kuwa inavisaka vipaji vya vijana kupitia sanaa ya maigizo, ambavyo vimejificha ili viendelezwe na kampuni yake. “Tumeamua kuwekeza katika sanaa maana sanaa ni fursa kama zilivyo fursa zingine nchini na ni matumaini yetu kuwa jamii itatuunga mkono katika safari ndefu tuliyo nayo ya kuvisaka na kuviendeleza vipaji,” anaeleza ofisa huyo uhusiano.
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions
Limited -
Dodoma
Hii ni baada ya washindi watatu kutoka Kanda
ya Kati kupatikana katika shindano la kusaka vipaji vya
kuigiza lililoendeshwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited
(PPL). Fainali ya kuvisaka vipaji kwa kanda ya Kati
ilifanyika jana Mnamo tarehe 15 April 2014 Mkoani
Dodoma na washindi kutangazwa na Jaji Mkuu wa shindano hilo,
Roy Sarungi aliyesaidiwa na Yvonne Chery
‘Monalisa’ na Single Mtambalike ‘Richie
Richie.’
Roy kwa kusaidiana na Yvonne Chery
‘Monalisa’ na Single Mtambalike ‘Richie
Richie.’ aliwatangaza Joyce Rebeca, Moses Obunde na
Mwinshehe Mohamed kuwa washindi wa shindano la kusaka vipaji
vya kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie
Talents ambapo kila mmoja alipewa zawadi nono ya Sh 500,000.
Shindano hilo liliwashirikisha washiriki 500, lakini ni
washiriki watano wenye vipaji waliofanikiwa kuingia tano
bora na baadaye majaji walifanya kazi kubwa ya kuwachagua na
kuwatangaza washindi
watatu.
Mshiriki mkubwa kuliko wote , Idrisa Ally
(40), alionesha kipaji cha hali ya juu cha kuigiza
na alizawadiwa na majaji Sh
100,000. Idrisa hatakwenda kushiriki
fainali za mashindano hayo zinazotarajiwa kufanyika
Agosti mwaka huu jijini Dar es Salaam kutokana na
umri wake kuwa mkubwa kuliko kigezo cha umri kilichowekwa
cha kuanzia miaka 14 hadi 35, ingawa majaji waliahidi
kuwasiliana naye kwa lengo la kuendeleza kipaji chake umri
wake
utakaporuhusu.
“Tumebaini kuwa Kanda ya Kati hususani
Mkoa wa Dodoma kuna vipaji vingi vya sanaa ya uigizaji na
katika hili Idrisa Ally ametuthibitishia
yeye ni mzee mwenye kipaji, lakini amedhihirisha kuwa ana
kipaji cha kuigiza,” anasema Jaji Mkuu wa
shindano hilo, Sarungi anasema sanaa ya uigizaji ni muhimu
kwa vijana, kwa vile sasa hutoa fursa ya ajira ambapo
imewawezesha vijana wengi nchini kujiajiri wenyewe na
kuimarika
kiuchumi.
“Ni matumaini yangu kuwa kwa washindi
hawa wa Kanda ya kati hawataishia hapa watajiendeleza zaidi
kwani uigizaji sasa ni ajira,” anasema.
Mshiriki Moses Obunde alishindwa
kuzuia furaha yake baada ya kutangazwa
mshindi, aliangua kilio kuashiria furaha aliyokuwa
nayo na kuufanya ukumbi mzima
kutaharuki.
Ofisa Uhusiano wa Proin Promotion Limited
(PPL), Josephat Lukaza, ambao ndio waratibu na waandaaji wa
shindano hilo la kusaka vipaji vya uigizaji, anasema
mashindano hayo yanaendeshwa kikanda, ambapo kwa kuanzia
walianza kusaka vipaji kwa Kanda ya Ziwa na Kumalizika Jana
katika Kanda ya kati Mkoa wa Dodoma na hatimaye zoezi hili
kuamia Kanda ya Juu Kusini ambapo usaili utafanyika Mkoani
Mbeya kuanzia tarehe 19
April.
“Baadaye tutaelekea Kanda ya Njanda za
Juu Kusini lakini tunashukuru kwa ushirikiano tulioupata kwa
wakazi wa Kanda ya Kati, tumepata washiriki 600, ambao
tuliwachuja hadi kuwapata washindi watatu waliokidhi vigezo
tulivyovihitaji,” anasema Lukaza. Baadhi ya vigezo kwa
mujibu wa Lukaza, vilikuwa ni mshiriki kuwa na umri kuanzia
miaka 14 hadi 35, anayejiamini, mbunifu, anayemiliki jukwaa
na igizo lake libebe ujumbe wa
kuelimisha.
Anasema lengo la PPL kuzungukia kanda hizo sita nchini ni kuhakikisha kuwa inavisaka vipaji vya vijana kupitia sanaa ya maigizo, ambavyo vimejificha ili viendelezwe na kampuni yake. “Tumeamua kuwekeza katika sanaa maana sanaa ni fursa kama zilivyo fursa zingine nchini na ni matumaini yetu kuwa jamii itatuunga mkono katika safari ndefu tuliyo nayo ya kuvisaka na kuviendeleza vipaji,” anaeleza ofisa huyo uhusiano.
Anasema PPL inaendesha shindano hilo kwa
kanda sita nchini ambazo ni Kanda ya Ziwa, Magharibi, Pwani,
Kati, Kaskazini na
Kusini.
“Kwa sasa tumeanza na mikoa sita,
lakini matarajio yetu ya baadaye ni kuifikia mikoa yote
nchini ambapo tunaamini kuna vipaji vingi vya wasanii
vimejificha ili waweze kupata ajira kupitia vipaji
vyao,” anasema na kuongeza kuwa mshindi wa jumla baada
ya mashindano ya kikanda kumalizika atapatikana Agosti mwaka
huu jijini Dar es Salaam, ambako ataondoka na zawadi nono ya
Sh milioni
50.
Anasema usakaji vipaji hivyo huendeshwa kwa
umakini na umahiri mkubwa kupitia kwa majaji na watu wenye
utalaamu wa tasnia ya filamu na teknolojia ya habari (IT)
walio chini ya kampuni yake, ambao pia huzingatia miiko na
maadili ya kazi hiyo kwa kila mshiriki. Anasema PPL
imesajiliwa rasmi mwaka 2013 kupitia Sheria ya Usajili wa
Makampuni ambayo hushughulika na ukuzaji wa sanaa ya filamu
nchini.
“Pia tunashughulika na usimamizi wa
uzalishaji wa filamu nchini, uzalishaji na usambazaji wa DVD
na filamu zilizokamilika kuingia sokoni na matarajio yetu ya
baadaye ni kuwa kampuni bora katika Bara la Afrika,”
anaeleza. Wakizungumza na gazeti hili, washindi waliobuka
kidedea waliwashukuru waandaaji wa shindano hilo kwa kuibua
vipaji vyao ambavyo wanasema visingeweza
kutambulika.
Crecensiah anasema anamshukuru Mwenyezi
Mungu kwa kumwibua katika shindano hilo na kumwezesha kuwa
mshindi, ambapo sasa anaamini kuwa ndoto yake ya kuwa msanii
wa kimataifa
imetimia.
“Namshukuru Mungu kwa yote, lakini zaidi niwashukuru waandaaji wa shindano hili kwa kutumia muda wao na fedha kuvisaka vipaji, binafsi naona kiu yangu ya kuwa muigizaji wa kimataifa imetimia, nitaongeza juhudi kubwa katika tasnia ya filamu,” anasema msanii huyo. Naye Janeth anasema penye nia pana njia, kwa madai kuwa alikuwa na kiu ya kuwa msanii wa kuigiza kwa muda mrefu hasa baada ya kuwaona wasanii mbalimbali kupitia luninga nchini.
“Namshukuru Mungu kwa yote, lakini zaidi niwashukuru waandaaji wa shindano hili kwa kutumia muda wao na fedha kuvisaka vipaji, binafsi naona kiu yangu ya kuwa muigizaji wa kimataifa imetimia, nitaongeza juhudi kubwa katika tasnia ya filamu,” anasema msanii huyo. Naye Janeth anasema penye nia pana njia, kwa madai kuwa alikuwa na kiu ya kuwa msanii wa kuigiza kwa muda mrefu hasa baada ya kuwaona wasanii mbalimbali kupitia luninga nchini.
“Kwa kweli naweza kusema nimepata maji
ya kunywa dhidi ya kiu yangu ya kuwa msanii, ni kazi ambayo
nilikuwa naipenda tangu nikiwa mtoto namshukuru sana Mungu
na waandaaji wa shindano hili la kusaka vipaji vya
kuigiza,” anaeleza mshindi huyo. Kwa upande wake,
Joshua Wambura anasema ushindi wake ni mwanzo wa safari yake
ndefu katika kuingia katika tasnia ya filamu ndani na nje ya
nchi.