Timu ya watoto wa Mitaani isaidiwe kikamilifu

Watoto hao wakiwa wamewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere
Wakonesha kombe juu

Wakilakiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juliana Yasoda

Hakika wanastahili pongezi

MOJA kati ya matukio muhimu na ya kutia moyo katika sekta michezo yaliyotokea kwa mwaka huu ni ushindi wa kombe la dunia uliotwaliwa na timu ya watoto wa mitaani.

Watoto hao kutoka kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Mwanza cha  (TSCSA) waliibuka na ushindi wa kombe la dunia kwa watoto wa mitaani uliofanyika nchini Brazil.


Katika fainali za mchezo huo watoto timu hiyo ya Tanzania iliifunga timu ya Burundi 3-0.


Binafsi mbali na kuungana na wadau mbalimbali wa michezo hapa nchini katika kuwapongeza watoto hao pia nina ushauri ambao naona unaweza kufuatwa katika kuhakikisha kuwa kile kilichofanywa na watoto hao kinaendelezwa.


Inaweza kuwa ni ngumu kwa watoto wale wale walioshinda michuano hii kuja kushinda tena michuano ya kombe la dunia la watoto wa mitaani lijalo lakini wanaweza kuwakilisha tena katika ngazi nyingine.


Nikisema kuwa sio rahisi kwa watoto wale wale kushinda kombe hilo nina maana kuwa mashindano hayo yanayofanyika kila baada ya miaka minne huenda wasiwe tena kwenye mazingira ya kushiriki kwa kuwa mashindano hayo ni kwa watoto wa mitaani na huenda wakawa sio tena wa mitaani.


Hapa nikiwa nina maana kuwa wanatakiwa kuanzia sasa hadi miaka mingine ijayo watoto hao wahakikishiwe kuwa wanatengenezewa mazingira ya kuinua uwezo wao wa kisoka na kushiriki katika ngazi nyingine.


Kwa kuwa wameonesha soka safi wakiwa watoto ni dhahiri kuwa wakiwekewa mikakati mizuri ya kukuza uwezo wao watajikuta wakilisaidia taifa hili miaka ijayo.


Kwa sasa wanatakiwa kuingizwa katika mfumo rasmi wa soka kwa kuanzia kushiriki michuano ya shule za msingi au sekondari.


Ili kuingia katika michuano hiyo inatakiwa wapelekwe shule na hivyo hapo linakuja suala zima la kusaidiwa ili kuwapeleka watoto hao shule.


Binafsi naona kuwa kwa kituo hicho kuwa kinawalea watoto hao kwa kuwafundisha soka na kisha watoto hao wanaendelea na shughuli zao wenyewe linaweza kubadilishwa na kwa sasa ikawa wanaelimishwa kwa kuwekwa darasani kabisa.
Kwa kupitia njia hiyo wanakuwa katika mazingira mazuri zaidi ya kufanya vema hata michezo kwa kuwa wanakuwa ni wachezaji wasomi.


Kipaji walichokionesha kwa sasa ni dhahiri kuwa kinapaswa kuendelezwa tena kwa njia na misingi endelevu ambayo inajumuisha elimu ya darasani pia.
Lakini ni wakati muafaka kwa  kituo hicho kuendelezwa kwa kuwekewa miundombinu ya kupata watoto wengine.


Inaonekana kuwa uongozi wa kituo hicho wanayo mikakati endelevu ya kufundisha soka na ndio maana wameweza kuibuka na ushindi huo.


Hivyo basi wanaweza kumbe kuwezeshwa na kutoa mafunzo ya soka  sio tu kwa watoto wa mitaani bali hata kwa watoto wengine pia.


Wapewe eneo kubwa lenye kuwa na karibia kila kifaa kinachotakiwa kutumiwa kwa ajili ya kufundishia michezo.


Mbinu wanazofundishi inatakiwa kuimarishwa pia ili kuibua vipaji vingi zaidi na hivyo inaweza hata kuwatoa watoto wengi walipo mitaani na wakaenda kujiunga na kituo hicho kwa lengo  la kukuza vipaji vyao.
============

Related

Sticky 8726451649488302618

Post a Comment

emo-but-icon

item