Ni Ngololo tena, sasa Diamond awania tuzo za watu, zinaendeshwa na Bongo5.com
https://habari5.blogspot.com/2014/05/diamond-kuwania-tena-tuzo-za-watu.html
Mwako wako huu |
Madam Nancy Mkurugenzi wa Bongo5.com ndio wanaleta sura mpya ya Awards hapa mjini |
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nasib Abdul, Diamond amechaguliwa tena kuwania tuzo za watu zinazoendeshwa na tovuti ya Bongo 5.com ambapo anawania kupitia kipengele cha Video Bora kupitia wimbo wake wa My Number One.
Katika kipengele hicho anashindana na wasanii wengine kama vile Ben Pol ambae anawania kupitia wimbo wake wa Jikubali, pia yupo msanii Mirror kupitia video yake ya Baby, Love Me ya Izzo Bizness akimshirikisha msanii Barnaba na Shaa, Muziki Gani ya Nay wa Mitego akimshirikisha Diamond.
Diamond wimbo wake huo na video ndio vimemwezesha kufika anga la kimataifa zaidi ambapo mbali na kushinda tuzo mbalimbali za Kili kupitia iwmbo huo lakini pia video ya wimbo huo imemwezesha kuwania tuzo ya MTV na BET.
Akizungumza na waandishi wa habari Mhariri Mkuu wa tovuti hiyo, Fedrick Bundala alisema kuwa wananchi wengi wamechagua wawapendao kushinda katika vipengele mbalimbali vya tuzo vilivyotangazwa kuwaniwa katika tuzo hizo.
Kwa upande wa mwongozaji wa Video anaependwa wanaowania tuzo ni pamoja na Nisher, Adam Juma, Nick Dizzo, Mecky Kaloka, Jerry Mushala
Video ya mwanamuziki wa kike inayopendwa zinazoshindanishwa ni pamoja na ile ya Amani ya Moyo ya Feza Kessy, Closer ya Vanessa Mdee, Sugua Gaga ya Shaa, Yahaya ya Lady Jaydee, Nakomaa na JIJI ya msanii Shilole.
Muigizaji wa kike wa filamu anaependwa wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, Jacqueline Wolper, Shamsa Ford, Irene Uwoya, Wastara Juma.
Kwa upande Muigizaji wa kiume anaependwa
wanaowania tuzo ni pamoja na Jacob Stephen, JB, King Majuto, Vincent Kigosi, Ray, Hemedy Suleiman, PHD, Salim Ahmed, Gabo.
Bundala alisema kuwa filamu inayopendwa ni pamoja na Foolish Age ya Elizabeth Michael, Lulu, Bado Natafuta ya Salim Ahmed pamoja na Shamsa Ford, Shikamoo Mzee ya JB, Shamsa Ford na King Majuto, Ndoa Yangu ya Kanumba, Wolper pamoja na Zawadi Yangu ya JB na Irene Uwoya.
Bundala alianza kwa kutaja kipengele cha mtangazaji wa redio anaependwa ambapo wanaoshindanishwa ni pamoja na Vanessa Mdee wa Choice FM, Millard Ayo wa Clouds FM, Hamis Mandi maarifu kama B12 wa Clouds FM, Mariam Kitosi wa Times FM na Ergon Elly wa Mbeya Highlands FM.
Bundala alisema kuwa kwa upande wa kipindi cha radio kinachopendwa vipindi vinavyogombaniwa ni pamoja na kipindi cha Xxl cha Clouds FM, Amplifaya cha Clouds FM, Hatua Tatu cha Times FM pamoja na Power Breakfast- Clouds FM.
Kwa upande wa mtangazaji wa runinga anaependwa wanaoshindanishwa ni pamoja na Salama Jabir na Sam Misago wa East Africa Television, pia yupo Zamaradi Mketema wa Clouds Tv, Salim Kikeke wa BBC Swahili na Gondwin Gondwe wa ITV.
Kipindi cha Luninga kinachopendwa Friday Night Live, Mkasi, Planet Bongo, na Uswazi vya East Africa Television na Take One cha Clouds TV.
Kwa upande wa wanamichezo wanaowania ni pamoja na Juma Kaseja wa Yanga, Mrisho Ngassa wa Yanga, Mbwana Samatta wa TP Mazembe, Ramadhan Singano wa Simba SC na Francis Cheka ambae ni bondia.
Bundala aliendelea kufafanua kuwa wananchi wanatakiwa kuchagua jina moja kutoka katika majina matano ya kila kipengele kilichotajwa.
"Wiki moja baada ya majina ya washiriki watano kutangazwa, mchujo wa kwanza utafanyika katika kila kipengele na kati ya wanaowania,mmoja ataondolewa na kubakiza wanne"alisema Bundala.
Aliongeza kuwa "Wiki moja baada ya mchujo huo wa kwanza, mchujo wa pili utafanyika na kuwabakiza wanaowania watatu kwenye kila kipengele".
Aliwataka watanzania kuwapiga kura wale wanawapenda kwa kutuma ujumbe mfupi wa neno TUZO kwenda 15678 na baadaye kufuata maelekezo rahisi ya kupiga kura pia kupitia tovuti www.tuzozetu.com.
==============================