Wasanii zingatieni aliyowaambia Wakuambiana
https://habari5.blogspot.com/2014/05/wasanii-zingatieni-aliyowaambia.html
HIVI majuzi tasnia ya filamu hapa nchini ilipata pigo kubwa ambalo ni kufuatia kifo cha msanii na mtayarishaji mkubwa wa filamu Adam Kuambiana.
Kuambiana alifariki dunia ijumaa iliyopita baada ya kuugua gafla na kisha kupoteza maisha akiwa kwenye hospitali ya TMJ.
Kifo hicho kilimkuta wakati akiwa kwenye juhudi zake za kila siku ambapo alikuwa akiendelea na utengenezaji wa filamu.
Kuambiana atakumbukwa zaidi kwa umakini wake wa kazi hasa akiwa kwenye uigizaji ambapo alionekana ni mtu ambae wakati akiwa katika uigizaji alikuwa akijua nini anachokifanya.
Ameshirikishwa kwenye filamu nyingi za wasanii wengine wakubwa lakini pia amekuwa akishiriki kwenye filamu hata za wasanii wa kawaida.
Kwa muda mrefu amekuwa akijishughulisha na suala zima la uongozaji wa filamu pia ambapo amekuwa ni mtu makini anaweza kuuvaa uhusika kwa kila namna.
Kifo chake kimekuja wakati jamii nzima ya watanzania wapenda filamu, waigizaji na hata wafanyabiashara ya filamu wamekuwa wakiuhitaji mchango wake katika tasnia hii.
Aliwahi kuliambia gazeti hili kuwa anataka siku kuona tasnia ya uigizjai ikiheshimiwa kama tasnia nyingine.
Katika mazungumzo hayo alisema kuwa ili kuipa hadhi inayostahili tasnia hiyo inatakiwa wasanii wenyewe kwanza kujitambua.
Pia alisisitiza kuwa ili wasanii wajitambue inatakiwa pia wazingatie suala la elimu ili angalau kukuza uelewa wao wa mambo zaidi.
Anasema kuwa kupitia elimu wasanii wanaweza kujisimamia kazi zao na pia kujua hata thamani yao na kazi zao wanazozifanya kwa ujumla.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Fenela Mukangara alieongoza maelfu ya waombolezaji waliojitokeza kwenye Viwanja vya leaders kuuaga mwili wa aliekuwa mwigizaji wa filamu marehemu Adam Kuambiana anaonesha ni kwa kiasi gani msanii huyo alikuwa muhimu.
Katika hotuba yake Fenella anawataka wasanii kuendeleza mazuri yaliyokuwa yakifanywa na marehemu Kuambiana na kuendeleza tasnia kwa ujumla.
Anasema kuwa marehemu alikuwa mtu mwenye kuipenda fani yake na alikuwa akiifanya kiuangalifu mkubwa kuanzia kuigiza hata katika kuongoza filamu.
"Mbali na kuwa msanii wa kuigiza lakini pia alikuwa akiongoza filamu na alikuwa mwalimu mzuri kwa wasanii wenzake, alikuwa na shauku ya kuona makubwa yakifanyika katika filamu hii na kwa sasa hakuna ubishi kuwa kazi yake inaonekana"alisema Fenella.
Pia Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fisoo anasema kuwa marehemu alikuwa ni mtu mwenye ushirikiano na kila msanii pamoja na uongozi mzima wa bodi ya filamu.
Anaongeza kuwa amendoka wakati tasnia ikiwa inamuhitaji zaidi hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko makubwa ya tasnia ya filamu.
Msiba huo pia ulihudhuriwa na wanasiasa ambapo msemaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Paul Makonda anasema kuwa marehemu alikuwa mfano wa uwajibikaji kwa vijana.
Anaongeza kuwa marehemu alifungua na kuimarisha ajira kwa vijana kujiingiza katika tasnia ya uigizaji wa filamu.
Kuambiana alikuwa na uhusiano wa karibu kabisa na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Stara Thomas ambae katika siku ya kuuaga mwili wa Marehemu aliimba nyimbo za kuaga mwili huo.
Akizungumza na gazeti hili anasema kuwa marehemu alikuwa na mchango mkubwa wa mawazo kwake uliomsaidia maisha yake ya muziki.
Anasema kuwa alikuwa ni mtu ambae hasifii umaarufu wake na wala alikuwa hana sifa licha ya kuwa alikuwa ni msanii mkubwa.
Anasema kuwa wasanii wengi wa sasa wanatakiwa kuendeleza yale aliyoyafanya kuambiana kwa kuhakikisha kuwa wanaipeleka tasnia hiyo mbele zaidi.
Msiba huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo hata wanasiasa pia ambao walionesha kusikitishwa kwao na msiba huo.
Mke wa marehemu ambae anaitwaa Janeth Rite ni diwani wa kata ya Kunduchi kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.
Kutokana na umahiri wake katika uigizaji ambapo alikuwa akiigiza masuala ya siasa imemfanya marehemu kuagwa hata na baadhi ya wanasiasa pia.
Ofisa habari wa Chadema Erasto Tumbo anatoa wimbo kwa wasanii kutoacha kuendeleza harakati za Kuambiana katika kuendeleza sanaa.
Anasema kuwa Kuambiana alikuwa akijitambua na alikuwa akifanya kila kile kinachitakiwa kufanywa na msanii kama kio katika jamii.
Watu mbalimbali waliohudhuria msiba huo walikuwa wakiangua kilio kila walipokuwa wakienda kuuaga mwili huo katika eneo la kuuagia.
Msanii wa filamu Jacob Steven, JB, alijikuta akianguka baada ya kuishiwa nguvu wakati alipokuwa akihojiwa kuhusiana na marehemu.
Mwili wa marehemu uliwekwa kwenye gari ambapo uliongozwa na wasanii kutoka katika viwanja vya Leaders hadi Makaburi ya Kinondoni.
Marehemu aliaga dunia Jumamosi iliyopita katika wakati akiwa katika shughuli zake za uigizaji wa filamu.
Marehemu Kuambiana amekufa akiwa na miaka 38, aliazaliwa Juni 6, 1976.
Moja kati ya filamu zilizomtambulisha msanii huyo katika ulimwengu wa sanaa ni filamu ya Fake Pastor ambayo aliigiza vema na kutetea hadhi yake katika filamu.