Toni Braxton akufuru Mungu
https://habari5.blogspot.com/2014/05/toni-braxton-akufuru-mungu.html
MWANAMUZIKI
wa Marekani, Toni Braxton amesema kuwa anaona kuwa ameadhibiwa na Mungu kwa
kuzaa mtoto mwenye ulemavu.
Alisema kuwa
akiwa kwenye umri wa miaka 31 alitoa mimba aliyopewa na mpenzi wake Keri Lewis.
Alisema kuwa
kilichopelekea kutoa mimba hiyo ni kwa sababu alikuwa katika hali mbaya
kiafyana hivyo asingeweza kuzaa mtoto kwa wakati huo.
Mwanadada
huyo aliewahi kutamba na wimbo wake wa I
am Break My Heart kwenye miaka ya 1994 aliongeza kuwa anaona kuwa kwa sasa
kuzaa mtoto mlemavu ni adhabu kutokal kwa Mungu.
"Mimi
nimezaliwa kwenye familia ya wazazi wakiwa watu wa dini tena sana na ninaona
kuwa kwa hili linalonipata kwa sasa linatokana na kushindwa kwangu kutambua
yale ambayo Mungu aliyakataza"alisema Toni Braxton.
Mtoto wake
huyo wa kiume aitwaye Diezel alikutwa na matatizo hayo mwaka 2006.