Mama yake Mzee Yusuph aibukia Bi Bomba
https://habari5.blogspot.com/2014/05/mama-yake-mzee-yusuph-aibukia-bi-bomba.html
Na Mwandishi Wetu
MAMA yake msanii wa muziki wa taarabu nchini Mzee Yusuph aitwae Mwanajuma Mzee ameibuka katika shindano la Bibi Bomba mwaka 2014 linalotarajiwa kuanza wiki ijayo.
Mama huyo aliechaguliwa akitokea kisiwani Zanzibar anaungana washiriki wengine waliopatikana juzi katika usaili wa mwisho uliofanyika katika viwanja vya Leaders Club kwa mkoa wa Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa shindano hilo linaloendeshwa na kituo cha Luninga cha Clouds Tv, Sakina Lyoka alisema kuwa waliopatikana katika mkoa wa Dar es salaam ni pamoja na Diana mushi, Zainab Habiti, Ruth Manfred na Sophia Shomari.
Alisema kuwa mabibi hao wataingia kambini wiki hii na akaongeza kuwa kwa mwaka huu wameongeza mikoa ya kuchukua washindani.
Alisema kuwa walizunguka katika mikoa sita nchini na kupata mwakilishi mmoja kutoka kila mkoa ambao wataungana na washiriki wanne kutoka Dar es Salaam na kuingia kambini wiki ijayo.
Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Mtwara ambao mshindi wake ni Mwanashuru Hoga, Mwanza ikiwakilishwa na Annastazia Chombo, Sulaiya Mahamoud kutoka Dodoma, Marium Ligaya kutoka Morogoro, Bi Moyo kutoka Tanga na Mwanajuma Mzee kutoka Zanzibar.
Alisema lengo kuwa la shindano hilo ni kupata bibi anayejielewa na mjanja lakini kuwbwa ikiwa ni kuwaweka pamoja mabibi hao na kujiona bado wanayonafsi katika jamii.
“Tumeamua kufanya hayo kwa kutafuta mabibi wenye vijpaji tofauti ili hata wakiwa kambini waweze kubadilishana mawazo, ndiyo maana tumeanza kuchukua mabibi wenye umri wa kuanzia miaka 50 na kuendelea” alisema.
=======================