Mashine za Umeme wa jua kukabili tatizo la maji
https://habari5.blogspot.com/2014/05/mashine-za-umeme-wa-jua-kukabili-tatizo.html
Na
Mwandishi Wetu
WASAMBAZAJI
wa vifaa vya umeme na maji katika Kanda ya
Africa
Mashariki, Davis & Shirtliff Group wameshauri Watanzania kutumia mashine
zinazotumia
umeme wa jua kukabili tatizo la uhaba wa maji na umeme.
Akizungumza
katika maonyesho ya 17 ya Build Expo 2014 Dar
es
Salaam juzi, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Davis & Shirtliff, Benjamin
Munyao
alisema suluhisho pekee la uhaba wa maji na umeme katika maeneo mbalimbali
nchini
ni kutumia umeme wa jua kuzalisha maji na umeme.
Alisema
robo tatu ya Tanzania
ni
kame na ni vigumu kwa watu kupata fursa ya kufikia maji safi hususani kwa
watu
walio mbali na bahari au maziwa.
Nanyaro
alisema,
ingawa Tanzania ina taasisi, sera na kanuni nzuri za kusimamia masuala
ya
maji, bado inakabiliwa na umasikini unaohusiana kwa njia moja au nyingine na
ukosefu
wa maji katika maeneo mbalimbali nchini.
“Davis
& Shirtliff wasambazaji wakubwa wa
vifaa
vya umeme na maji wamejikita katika sekta sita za bidhaa zao ikiwemo
pampu
za visima vya maji, ambapo kupitia bidhaa mbalimbali kama Dayliff, Sundaya,
Opti,
Grundfos
na Shurfloni suluhisho la ukosefu wa maji na umeme.
Lorentz
- pampu inayozalisha maji kwa kutumia
mionzi
ya jua ilikuwa moja ya vifaa vilivyovutia katika maonesho ya 17 ya Build Expo
2014
kutokana na muundo wake unaodhibiti na kutenga
kiwango
cha chininacha juuchakasi ya maji.