Kikosi cha England chawekwa hadharani

KIUNGO Ross Barkley ni mmoja kati ya wachezaji 23 waliochaguliwa kuwakilisha timu ya England kwenye michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika mwezi ujao nchini Brazil.
Pia anakuwa na mchezaji mwenzake John Stones anaechezea klabu ya Everton.


Barkley (20) anaungana wachezaji wengine akina wa timu ya Southampton  Rickie Lambert, Adam Lallana na Luke Shaw. 


Kikosi hicho kilitangazwa jana na kocha mkuu wa timu hiyo Roy Hodgson am,bapo kina wachezaji akina Michael Carrick wa Manchester United na Ashley Cole wa Chelsea wameachwa kwenye kikosi hicho.


Timu hiyo ya England itaumana na Italia katika mchezo wake wa kwanza utakaochezwa Juni 14, kaika kujiandaa na mchezo huo itaumana na Peru Mei 30 ikiwa ni mchezo wa kirafiki. 


Kwa mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa ifikapo Juni 2, ndio itakuwa mwisho wa kutangazwa kwa wachezaji watakaowakilisha kila nchi katika michuano hiyo ya Kombe la Dunia.


Kikosi hicho kimetoa ratiba yake ya mechi za kirafiki ambapo Juni 4 itacheza dhidi ya  timu ya Honduras mchezo utakaofanyika jijini  Miami, Marekani. 


Pia Juni 7 itaumana na Ecuador hapo hapo Miami Marekani, itaanza mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Dunia dhidi ya Italia Juni 14.


Michezo yake mingine ni mchezo wa Juni 19 dhidi ya Uruguay jijini Sao Paulo, Juni 24 atacheza dhidi ya Costa Rica katika jiji la Belo Horizonte 


Kwa upande wa makipa waliochaguliwa ni Joe Hart (Manchester City), Ben Foster (West Bromwich Albion), Fraser Forster (Celtic).
Kwa upande wa mabeki Hodgson amewachagua akina Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), Phil Jones (Manchester United), Luke Shaw (Southampton), Chris Smalling (Manchester United).

Hodgson amewachagua viungo akina Ross Barkley (Everton), Steven Gerrard (Liverpool), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Southampton), Frank Lampard (Chelsea), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Raheem Sterling (Liverpool), Jack Wilshere (Arsenal).

Washabuliaji ni pamoja na Rickie Lambert (Southampton), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Danny Welbeck (Manchester United).

Hodgson kwa upande wa wachezaji wa akiba amewachukua akina John Ruddy (Norwich City), Jon Flanagan (Liverpool), John Stones (Everton), Michael Carrick (Manchester United), Tom Cleverley (Manchester United), Andy Carroll (West Ham United), Jermain Defoe (Toronto FC).


Pia Beki wa Jon Flanagan (21) anaungana na kipa wa Norwich John Ruddy, pia yupo mshambiliaji wa timu ya West Ham Andy Carroll, pia yupo mshambuliaji wa timu ya Toronto Jermain Defoe.


Kiungo wa  Carrick, Tom Cleverley na beki wa Stones wanaungana katika kikosi hicho.


Wachezaji wengi wa timu ya Liverpool wamechaguliwa kwenye kikosi hicho ikilinganishwa na timu nyingine.

Kipa wa timu ya West Brom, Ben Foster amechaguliwa pamoja na mwenzake kutoka timu ya Celtic, Fraser Forster wakiwa wanamwakilisha kipa Joe Hart.


Foster amekuwa nje ya soka kwa muda mrefu kuanzia May 2011 na February 2013 na hajawakilisha katika timu hiyo ya taifa tangia mwaka 2010. 


Pia Hodgson amemchukua winga wa Liverpool Raheem Sterling, pia  kiungo Jordan Henderson,  beki wa Manchester United Phil Jones, pia Alex Oxlade wa Arsenal  pamoja na Jack Wilshere wote wamechukuliwa katika kikosi hicho.

Pia kiungo wa Chelsea Frank Lampard (35) pamoja na Steven Gerrard (33) Phil Jagielka (31) Lambert (32), na Foster(31) hao ni kwa wachezaji walio na umri wa zaidi ya miaka 30.


Mchezaji wa Arsenal, Oxlade-Chamberlain amechukuliwa licha ya kuwa hajacheza tangia April 20 kutokana na kukabiliwa na majeraha ya goti lakini mchezaji mwenzake Wilshere amechukuliwa ila kwa yeye ameshapona.


Wachezaji akina Wayne Rooney (28) wa Manchester United pamoja na  Jones (22) wamechukuliwa pia kwenye kikosi hicho licha ya kuwa wamekuwa wakikabiliwa na majeraha yaliyowafanya hata wakakosa kuchezea timu zao kwenye michezo yao ya mwisho yaLigi Kuu.

Related

Sticky 1914211723626604792

Post a Comment

emo-but-icon

item