Baiskeli mchezo unaotumiwa kuhamasisha maendeleo na mabadiliko katika jamii.

                                                                           
Lelo akiwasili mkoani Arusha

Alipokelewa na waendesha baiskeli mkoani hapo


Huyu ni mwendesha baiskeli kutokea nchini India akikaribishwa Ubalozi wa India

Akizungumza na waaandishi wa habari


Akiagwa na Balozi

Na Mwandishi Wetu
BAISKELI kwa mara hutumiwa kama chombo cha usafiri ambacho watu hutumia kutoka sehemu moja kwenda nyingine.


Ni kama ilivyokuwa kwa gari ambalo nalo hutumiwa mara nyingine kusafiria kutoka sehemu moja kwenda nyingine.


Lakini pia mbali na baiskeli kuwa chombo cha usafiri pia kinatumika kama chombo kwa ajili ya michezo mbalimbali.


Wapo wanaotumia baiskeli kama kifa cha kuburudishia hasa kwa kutumia kwa kuoneshea aina mbalimbali za uendeshwaji wake.


Hapa nawagusa wale ambao wanaonesha shoo mbalimbali za uendeshwaji wa baiskeli wakiwa wanakimbia nazo na kuruka nazo juu huku wakionesha madoido mbalimbali.


Kifaa hiki kwa miaka ya hivi karibuni kimekuwa kikitumiwa kama chanzo cha kueneza ujumbe kuhusiana na masuala mbalimbali ndani na nje ya nchi.


Wapo wanaosafiria umbali mrefu wakitumia baiskeli hiyo kueneza ujumbe wa dini, ujumbe wa masuala ya magonja na mengineo.


Hivi karibuni alirejea nchini Kijana wa Arusha Elvis Munis akitokea mataifa mbalimbali ambapo anasema kuwa kupenda kwake mchezo wa Baiskeli ndiko kulikopelekea kutumia kifaa hicho kueneza ujumbe kupinga masuala mbalimbali katika jamii.


Anasema kuwa kwake baiskeli sio tu kama mchezo au kama kifaa cha kawaida ila ni kifaa alichoanza kukitumia kwa kutambua nafais yake katika kufikisha ujumbe wake kwa jamii.


"Baiskeli kama baiskeli ni chombo cha usafiri kama vingine tunavyoona gari au vingine ila kwangu mimi nimekuwa nikichukulia kwanza kama mchezo awali na lakini baadae nimekuja kukitumia kuzunguka karibia dunia nzima"alisema Munis ambae maarufu anajulikana na Lelo.


Anasema kuwa anapenda michezo michezo mingine kama vile soka ambapo zamani alikuwa akipenda zaidi timu ya Yanga na kisha amekuja kutokea kupenda zaidi mchezo wa kukimbia.


Anasema kuwa alikuja kuona kuwa akitumia mchezo wa kuendesha baiskeli kueneza ujumbe wa kupambana na uharibifu wa mazingira na kuimarisha amani ataifikia jamii kubwa ya kitanzania na dunia nzima kirahisi zaidi.


Akizungumzia safari zake hizo alisema kuwa amerejea Tanzania akitokea Kenya na kabla ya hapo alikuwa Rwanda na alitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Kongo Brazaville.


Anaongeza kuwa awali ziara yake hiyo iliyokuwa na mikikimikiki mingi ilianzia katika eneo la Arusha hapo nchini Misri na kisha Sudan, Ethiopia, Angola, Lesotho, Swazland na Rwada kisha Burundi.


Anasema kuwa baada ya hapo alielekea nchini Argentina,Chile,Brazil,Colombia,Venezuela,Mexico, Marekani Ureno na Canada.


 "Ni safari yangu ambayo imetokana na mchezo huu wa baiskeli lakini kwa sasa inaonekana kuwa inaleta mabadiliko katika jamii hasa kwa pale inaposambaza ujumbe wa mapambano kwa ajili ya uimarishaji wa mazingira, kukusanya ada ya shule kwa watu wasiojiweza na kudumisha amani"anasema kijana huyo.


Ameanza ziara yake hiyo tangia mwaka 2009 na kwa sasa imeshafika miaka mitano ndio anamaliza zaiara yake hiyo ya aina yake.


Lelo pia alifika nchi za Norway, Sweden, Ujerumani, Denmark, Uholanzi ,Ubelgiji, Ufaransa, Hispania, Luxemberg.


Anaongeza kuwa lengo lilikuwa ni kukusanya milioni 120 na kwa sasa ameshapata milioni 30 na anaweza kujisifia kuwa ametumia miaka mitano kukusanya fedha kwa kutumia baiskeli na kuisaidia jamii yake.


Anawataka vijana kujiamini na kutumia fani walizonazo katika kuleta mabadiliko kwenye jamii inayozunguka bila ya kukata tamaa.


Anasema kuwa aliwahi kuibiwa baiskeli yake akiwa anaendelea na juhudi zake za kutafuta fedha hizo za kusaidia jamii yake ya kitanzania.


"Huu ni kama mfano kwa vijana wengine, mfano tuangalie hata katika jamii ya wachezaji wanaweza kutumia mchezo huo kuandika historia katika jamii kwa kwenda mbali kutafuta mafanikio kwa jamii ya kitanzania"alisema Lelo.


Anaongeza kuwa"kwa upande wangu mimi niliona baiskeli kama mchezo kwanza lakini nikachukulia ni kama kifaa kazi muhimu kwangu na kwa maisha ya wengine na leo nimetimiza kazi na adhma yangu hii."


Katika kuunga mkono kazi na adhma hiyo ya Lelo katika kutumia baiskeli kwenye kuleta mafanikio kwa jamii yake, kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imemuunga mkono.


Meneja wa Mawasiliano na Mahusiano wa Tigo John Wanyancha anasema kuwa kampuni hiyo imetambua nafasi ya Lelo kama kijana anaetaka kuleta mabadiliko kwa jamii yake na imeamua kumuunga mkono kwa kazi yake hiyo.


Pia Jumatano iliyopita hapa nchini alishuhudiwa mwendesha baiskeli kutokea nchini India, Somen Debnath ambae ametumia miaka 10 kuzunguka dunia.


Debnath anasema kuwa amekuwa akitumia baiskeli kueneza ujumbe dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi ambapo amekuwa akiwataka watu kuwapenda na kuwatunza waathirika.


Anafafanua kuwa akiwa kama mpenzi wa mchezo wa Baiskeli anakitumia chombo hicho kwa mtazamo wa pili zaidi ambapo ni kueneza ujumbe wa kupambana na masuala ya afya.


Akizungumza na gazeti hili katika, mwendesha baiskeli huo anasema kuwa alikuwa na ndoto ya kutumia baiskeli kama mchezo na umsaidie kuwakilisha India kimataifa zaidi.


Anaongeza kuwa hata hivyo ndoto yake hiyo ilikuja kufutika baada ya kuona mwathirika akitengwa na jamii yake yake na ndipo akaanza ziara ya kutumia chombo hicho kusafiria kila kona ya dunia kueneza ujumbe wa kupambana na ugonjwa huyo.


Amefika Dar es salaam akitokea Burundi kupitia mkoa wa Kigoma na ametumia siku nane kufika Dar es salaam huku njia akikutana na vitu mbalimbali ambavyo anadai kuwa ni pia fundisho kwake.


Akiwa hapa nchini kwa siku kumi atazitumia kujadiliana na watu mbalimbali kuhusiana na mchezo wa baiskeli pamoja na namna ya kushirikiana nao kupambana na ugonjwa wa ukimwi.

   

Related

Sticky 4920674290629590846

Post a Comment

emo-but-icon

item