Shule ya Muziki ya Music Mayday imezinduliwa rasmi, ipo MIkocheni

Kwa nje kulikuwa na kundi la sarakasi

Baada ya hapo tukaingia ndani

Wanafunzi wa Music May day wakiimba 

Wadau mbalimbali wa sanaa walikuwapo kulia ni Mkurugenzi wa Sanaa wa Kituo cha Babawatoto, Mgunga Mwa Mnyenyelwa

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza (kushoto) Meneja Mradi wa Music Mayday Hildegard Kiel

Kuna vifaa vya kisasa kama studio ya kujifunzia kurekodia muziki

Mngereza akijaribu kifaa kimojawapo

Maregesi ambae pia ni ofisa kutoka Basata akapata wasaa wa kupiga gitaa

Akaendelea na kwenye piano




Katika shule hiyo pia kuna eneo maalum la kulala wageni wakifika shuleni hasa kwa wale wataalamu wa muziki kutoka nje ya nchi

Ni pakubwa haswa

Kundi la 909 lilikuwapo

The Voice pia waliwakilisha
Na Evance Ng'ingo
WAZAZI wametakiwa kuwaendeleza watoto wao katika elimu ya muziki ili waweze kuitangaza nchi na kupanua wigo wa ajira kupitia tasnia hiyo.


Wito huo ulitolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza wakati akifungua rasmia mafunzo ya muziki katika Shule ya Muziki ya Music Mayday.
Mngereza alisema kuwa kwa sasa muziki ni kazi rasmi na watu wamekuwa wakiwekeza zaidi kwenye fani hiyo inayokuwa kwa kasi hapa nchini.


Alisema kuwa kupitia muziki wananchi wamekuwa wakipewa elimu yakutosha kutokana na masuala mbalimbali na hivyo kutimiza ile dhana ya kuwa muziki ni shule kamili inayoelimisha na kuwataka wasanii kujiendeleza kwenye elimu ya muziki.


Kwa upande wake Meneja Mradi huo wa Music Mayday Hildegard Kiel alisema kuwa kwa sasa shule hiyo ina wanafunzi 60.


Alisema kuwa wanafunzi hao 60 wapo chini ya udhamini wa masomo wa miaka miwili.


"Hawa wanafunzi wanaosoma hapa ni wale waliopatikana katika mashindano ya wazi yaliyofanyika Temeke, Mwenge na Masaki na wanafundishwa muziki wakiwa hapa."alisema Hildegard.

===================

Related

Sticky 2575804940988009504

Post a Comment

emo-but-icon

item