Bang Magazine yagonga miaka 10, yafanya sherehe, The Voice yaburudisha vema

Elgiver alifungua mvinyo
The Voice waliwakilisha
Mwanamuziki Yvone Sangudi ambae ni Mtanzania anaefanya shughuli zake za muziki Marekani alikuwapo
Mtoto anaimba huyu

Emelda Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Relim inayomiliki jarida la Bang (mwenye nyeusi) akijimwaga mwaga

Akiwa na friend

Pamoja na friends
Na Evance Ng'ingo
MSANII wa kitanzania aishie nchini Marekani Yvonne Sanguda pamoja na kundi la muziki wa Injili la The Voice juzi walifanya onesho zuri kwenye sherehe za kuadhimia miaka 10 ya jarida la Bang.


Katika sherehe hizo zilioandaliwa na kampuni ya Relim inayomilikia jarida hilo zilifanyika katika fukwe ya Escape One na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.


Msanii Yvonne alianza kwa kuimba nyimbo zake kadhaa huku akiwa anacheza na kuimba kwa pamoja na  kuonesha uwezo wa hali ya juu katika kumudu jukwaa.


Aliendelea kucheza huku akiimba na kuna wakati alikuwa akikaa chini kwenye steji ambapo alikuwa akiimba muziki wa live akisaidiwa na bendi ya Tanzanite.


Baada ya hap likaja kundi la The Voice ambalo linaundwa na wasanii sita ambao waliomba wimbo maalum wa kulipongeza jarida hilo.


Walizikonga nyoyo za wageni waliohudhuria onesho hilo hasa kutokana na umahiri wao wa kuimba bila vifaa ila wakijitungia mapigo ya muziki wenyewe (Akapela).


Mwanadada Angel Magoti wa kundi hilo alikuwa ni mfano wa kuigwa kutokana na umakini wake katika kupanga sauti na kuimba kwa ufahasa.


Aliimba wimbo wa I Will Always Love you ambapo alijikuta akipewa zawadi kadhaa kutokana na umakini wake katika kuimba.


Jarida la Bang lilianzishwa mwaka 2004 ambapo limekuwa likijihusisha na kusaidia wasanii pamoja na masuala mengine katika jamii.


Mkurugenzi wa Jarida Hilo Emelda Mwamanga alisema kuwa kwa miaka 10 limesaidia mengi katika tasnia ya michezo, sanaa na mengineo.
================================

Related

Simba yapigwa faini

BODI  ya Ligi Kuu Tanzania  bara (TPLB) imeipiga faini  klabui ya Simba ya jumla ya sh. milioni moja  kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo vitendo vinavyoashiria ushirikina uwan...

Stamico yafagilia ulinzi wa JKT mgodini

SHIRIKA la Uzalishaji Mali  la Jeshi la Kujenga Taifa,  SUMA JKT, limepongezwa kwa juhudi zake katika kuhakikisha ulinzi unaimarika katika maeneo ya mgodi wa STAMIGOLD uliopo Biharamulo Ka...

Kidume chenye mvuto Marekani

Jaji wa shindano la kuimba ya NBC singing show juzi alitajwa kuwa ni mwanaume mwenye mvuto zaidi kupitia jarida la People Magazine. Jamaa huyo ni mwanamuziki Adam Levine  ni kijana huyo wa m...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

item