The Voice --tunaifikia jamii kwa nyimbo za Injili



Kundi la Muziki wa Gospel la The Voice limesema kuwa litaendelea kutoa elimu zaidi ya Mungu kwa njia ya muziki.


Kundi hilo mwaka huu linatimiza miaka 20 tangia kuanzishwa kwake.


Kundi hilo linaloundwa na wanamuziki kutoka ukoo mmoja lilianza kufanya kazi zake za muziki tangia wakiwa watoto mwaka 1994 .


Akizungumza na safu hii Meneja wa kundi hilo, Obed Mark alisema kuwa wakiwa wanatimiza miaka 20 tangia kuanza kuimba wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufikia idadi kubwa ya watu wa rika mbalimbali.


Alisema kuwa wanaimba muziki wa Injili wakitumia vionjo mbalimbali na wamekuwa wakipata mialiko kwenda katika hafla mbalimbali.


"Sisi kama unavyotuona tunaonekana kuwa ni bado wadogo kiumri sasa tukisema tunaadhimisha miaka 20 inamaanisha ni kuanzia pale tulipoanza kuimba tukiwa watoto na kwa sasa tunazidi kukua kwa kuongezeka pia hata kwenye kundi"alisema Mark.


Wanaounda kundi hilo ni pamoja na Obeid Mark, Mark Mark, Daniel Mark, Baraka Mark, Josia Bedock na Josia Magoth.

Related

Makala: Jisomee kuhusiana na tuzo za Kili

Diamond na Wema HIVI majuzi zilifanyika tuzo za muziki za Kilimanjaro Tanzania Music Award 2014 (KTMA) ambapo zilifana na kushuhudiwa wasanii wengi wakichukua tuzo zao. Ilikuwa ni katika ukumb...

Jicho la Habari5blog katika Kili Awards 2014

                                 &...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

item