Hapana chezea Lady in Red Show
http://habari5.blogspot.com/2014/02/ilivyokuwa-jana-katika-shoo-ya-lady-in.html
Miss Tanzania kwa mwaka 2013 na 2014 Hapiness Watimanywa |
Asia Mwandaaji wa onesho hilo |
Mbunge wa Bunge la Katiba akihojiwa na Deo wa Nivana wa East Afrika Television |
Asia akimkabidhi ua mumewe |
Mdau wa Swahili Fashion akiwa na Miss Tanzania |
Huyu dada ni mbunifu kutokea mkoani Dodoma kuna habari yake ndefu itakuja keshi mchana hapa hapa kwenye blog hii, Usikose |
Michuzi akiwa na mkewe |
Dah kweli Mkuu anapenda kazi yake alikiwa pia akichukua Video |
Akishow love akiwa na mkewe na mdau mwengine |
Martin Kadinda kushoto alionesha kazi yake |
Asia akiwa na mumewe jukwaani, kushoto ni Miss Universe |
Mkewe Michuzi akichukua picha ambayo kampuni ya Michuzi Media Group iliinunua ikiwa ni mchango kwa waathiri wa dawa za kulevya. |
Burudani safi ilikuwapo |
Vyeti vilitolewa hapa ni mwakilishi wa Darling Rasta akipokea cheti kutoka kwa Maria Sarungi |
Mkewe Michuzi akichukua cheti kutoka kwa Maria aliekuwa mgeni rasmi siku hiyo |
Anaechukua cheti kwa sasa ni Export Co-Ordnator wa TDL Bavon Ndumbati, ambapo kampuni hiyo ilidhamini kupitia kinywaji chake cha Zanzi |
Rio Paul |
Onesho la Mavazi la Lady in Red lilifanyika jana ambapo liliendana sambamba na sherehe ya siku ya wapendanao, Valentine Day.
Onesho hilo lililotimiza miaka 10 hiyo jana lilifanyika katika hoteli ya Serena kwa udhamini mkubwa wa kinywaji cha Zanzi, Rasta za Darling, Michuzi Blog pamoja na wadau wengine.
Ilikuwa ni onesho zuri lililowakutanisha pamoja wabunifu wakongwe wa mitindo pamoja na wabunifu chipukizi na pia iliendana sambamba na mnada kuchangisha fedha za kuwasaidia waathirika wa madawa ya kulevya.
Katika shoo hiyo pia kulikuwa na burudani safi kutoka kwa msanii Wanne Star pamoja na Nyemo ambapo walizikonga nyoyo za watu waliohudhuria mahalahapo.
Mmiliki wa Michuzi Media Group Issa Michuzi katika kuonesha upendo kwa siku hiyo kwa waathirika wa dawa za kulevya alinunua picha moja kwa milioni moja na elfu kumi ikiwa ni kama sehemu ya mchango wake.