Ikiwa zimebakia siku kadhaa 28 kuelekea kombe la Dunia Brazil
https://habari5.blogspot.com/2014/05/ikiwa-zimebakia-siku-kadhaa-28-kuelekea.html
KOCHA wa timu ya taifa ya Greece, Fernando Santos amekitaja kikosi cha nchi hiyo kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia mwezi ujao nchini Brazil.
Waliochaguliwa ni pamoja na makipa Alexandros Tzorvas (Apollon Smyrnis), Orestis Karnezis (Granada), Panaglotis Glykos (PAOK), Stefanos Kapino (Panathinaikos)
Kwa upande wa walinzi waliochaguliwa ni pamoja na Avraam Papadopoulos, Kostas Manolas, Giannis Maniatis, Jose Holebas (all Olympiakos), Sokratis Papastathopoulos (Borussia Dortmund), Giorgios Tzavellas (PAOK), Loukas Vyntra (Levante), Vasilis Torosidis (Roma), Vangelis Moras (Verona), Nikolaos Karabelas (Levante)
Kocha Santos aliwataja wachezaji wengine kuwa ni pamoja na Alexandros Tziolis (Kayserispor), Andreas Samaris (Olympiakos), Kostas Katsouranis (PAOK), Giorgos Karagounis (Fulham), Panagiotis Tachtsidis (Torino), Ioannis Fetfatzidis (Genoa), Kostas Fortounis (Kaiserslautern), Lazaros Christodoulopoulos (Bologna) Panagiotis Kone (Bologna)
Washambuliaji waliochaguliwa ni pamoja na Dimitris Papadopoulos (Atromitos), Dimitris Salpingidis (PAOK), Giorgios Samaras (Celtic), Konstantinos Mitroglou (Fulham), Theofanis Gekas (Konyaspor), Stefanos Athanasiadis (PAOK), Nikos Karelis (Panathinaikos)
Katika kikosi hicho mchezaji wa Fulham, Konstantinos Mitroglou amejumuishwa kwenye kikosi cha Greece cha wachezjai 29 watakaowakilisha katiak michuano ya Kombe la Dunia itakayoanza mwezi ujao Brazil.
Mchezaji huyo hajaisaidia vya kutosha timu yake ya sasa ya Craven Cottage aliyoihamia akitokea timu ya Olympiacos mwezi Januari kwa kitita cha Pauni Milioni 11.
Ameichezea klabu hiyo kwa dakika 120 tu na kushindwa kuisaidia timu yake hiyo katika ligi kuu na kujikuta ikimaliza ligi hiyo vibaya.
Mbali na hali hiyo lakini kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, amesema kuwa anaona kuwa mchezaji wake huyo anayo nafasi ya kuitumikia timu kwenye michuano ya kombe la dunia.
==============================================
MCHEZAJI wa timu ya Manchester City, raia wa Ufaransa alieachwa kwenye kikosi cha timu yake ya taifa, Nasri, amesema kuwa ameamua kutafuta sehemu ya kupumzika itakayomwezesha kuondokana na mawazo ya kuachwa kwenye kikosi hicho.
Nasri alisema kuwa amekuwa kwenye wakati mhumu sana kwake wka sasa kutokana na kuachwa kwenye kikosi chake hicho.
Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps alitaja kikosi chake kamili kitakachowakilisha nchi hiyo mwezi ujao kwenye michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil.
Nasri mbali na kutotajwa kwenye nafasi 11 muhimu lakini pia hayupo hata kwenye kikosi cha saba watakaokuwa benchi kwa mabadilishano.
Alisema kuwa kwa sasa ni mara ya pili ameachwa kwenye chake cha timu ya taifa ambapo amekuwa akiwa na shauku ya kukitumikia kikosi hicho kwenye michuano hiyo kwa muda mrefu.
Alisema kuwa hakuna mchezaji yoyote duniani ambae anaweza kufurahia kuachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kinachocheza kwenye michuano muhimu mikubwa kama hiyo.
Alisema kuwa kwa upande wake anaona kuwa ni kama amekuwa akionewa kwa kutopewa nafasi ya kuitumikia nchi yake na kuongeza kuwa anaona ni kama anabaguliwa.
Deschamps alisema kuwa mchezaji huyo hayupo kwenye kiwango cha kwanza cha kuanza kuchezea timu hiyo na akaongeza kuwa hata mchezaji huyo mwenyewe aliwahi kukiri kuwa hayupo tayari kuwa mchezaji wa kusubiria kuingia kwa mabadilishano (sub) na hivyo ndio maana aliamua kumwacha kabisa.