Nipigeni tafu kuchukua tuzo nilizochaguliwa kushiriki
https://habari5.blogspot.com/2014/05/nipigeni-tafu-kuchukua-tuzo-nilizoshinda.html
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nasib Abdul, Diamond Platnum amewataka watanzania kutambua kuwa tuzo anazoshindania za MTV pamoja na BET ni tuzo za watanzania wote kwa ujumla.
Diamond ambae hivi majuzi alishinda tuzo saba katika tuzo za Muziki za Kilimanjaro alisema kuwa ni wakati kwa watanzania kumuunga mkono katika kushinda tuzo anazowania kwa sasa.
Alisema kuwa ni heshima kubwa kwake pamoja na watanzania wengine wote kwa ujumla kwa kuchaguliwa kuwania tuzo za MTV pamoja na tuzo kubwa na ya heshima zaidi duniani ya BET.
Msanii huyo ni msanii peke yake kuteuliwa kuwania tuzo ya MTV kwa kipengele cha wimbo bora wa kupitia wimbo wake wa My Number One alioimba na msanii Dovido wa Nigeria.
Pia anashiriki kwenye kipengele cha msanii bora wa kiume katika tuzo hizohizo huku kwenye tuzo za BET za Marekani anashiriki katika kipengele cha msanii bora wa kimataifa akiwa anatokea nje ya Marekani.
Kundi la Camp Muller kutoka Kenya lilichukua tuzo ya BET katika kipengele hicho na kwa sasa ni msanii Diamond pekee kutoka Afrika Mashariki kuchaguliwa kuwania kipengele hicho.
Diamond alisema kuwa iwapo akishinda tuzo hizo zote kuanzia za MTV na BET atatumia muda wake mwingi zaidi kuitangaza Tanzania kupitia tuzo hizo.
"Huu ni wakati wa sisi kuungana na kuhakikisha kuwa tunachukua tuzo hizo ambazo ni zetu sote kwa pamoja, hivyo tuombeane pamoja na kusaidiana kushinda kwa faida zetu sote"alisema Diamond.