2face anusurika katika ajali ya ndege
http://habari5.blogspot.com/2014/02/2face-anusurika-katika-ajali-ya-ndege.html
MWANAMUZIKI mahiri wa Nigeria, 2face pamoja na abiria wengine wamenusurika kufa kwenye ndege iliyopata hitirafu ikiwa angani.
Hiyo ni kufuatia mlango wa ndege hiyo kufunguka ghafla wakati ikiwa angani muda mchache baada ya kuruka.
Msanii huyo alietamba na wimbo wake a My African Queen aliuambia mtandao wa Nigeria Films kuwa alikuwa akisafiria shirika la ndege la Aero Contractors Flight Aj2002 akitokea jijini Lagos kuelekea Douala.
Alisema kuwa tukio hilo lilitokea siku ya wapendanao (February 14) na alijikuta akilazimika kufanya maombi kuomba Mungu awaepushe na ajali hiyo.
Ndege hiyo ilienda Nigeria kwa ajili ya matengenezo na kujikuta ikilazimika kubeba abiria kuwapeleka Douala.
"Ilikuwa ni kama dakika 30 baada ya ndege kuruka na hapo nilikuwa nimeshamaliza kula chakula na kupata kinywaji na ndio tukasikia tunaambiwa kuwa kuna mlango mmoja upo wazi hivyo tulitakiwa kuwa makini"alisema 2face.
Alisema kuwa ndege hiyo ililazimika kurejea tena Lagos na walitumia dakika 40 kurejea hadi Lagos na wakati huo ndege ilikuwa ikiruka usawa wa chini zaidi.
Alisema kuwa walipofika katika uwanja wa ndege wa Lagos walijikuta wakilazimika kusubiria ndege nyingine na aliomba mamlaka husika kuhakikisha kuwa wanaizuia ndege hiyo kutoruka tena.