Coca Coca kuendeleza burudani safi na bure kwa watanzania
http://habari5.blogspot.com/2014/02/coca-coca-kuendeleza-burudani-safi-na.html
Meneja Bidhaa wa Coca Cola Maurice Njowoka akifafanua zaidi kuhusiana na burudani hiyo |
Mcheki Vanessa alivyong'aa |
Na Mwandishi wa Habari5blog
WASANII kadhaa wa muziki wa Bongo Fleva Jumapili ijayo watatoa burudani katika onesho la wazi litakalofanyika katika fukwe ya Coco.
Wasanii watakaoshiriki onesho hilo lijulikanalo kama Good Time ya ukweli na Coca Cola ni pamoja na Madee,Vanessa Mdee,Joe Makini na Diamond.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Meneja wa Bidhaa wa Coca Cola waandaaji wa onesho hilo, Muirce Njowoka alisema kuwa onesho hilo ni la kwanza litakalofuatiwa na maonesho mengine ya bure mikoani.
Alisema kuwa pia Februari 22 itakuwa zamu ya mkoa wa Mwanza ambapo Diamond, TMK Wanaume Family pamoja na Madee.
Aliongeza kuwa Machi Mosi itakuwa zamu ya Arusha ambapo onesho litafanyika katika uwanja wa Soweto ambapo wasanii kama vile Jambo Squad, Vanessa Mdee na Joe Makini watatoa burudani.
Aliongeza kuwa Machi 8 jijini Mbeya itafanyika onesho la wazi la katika Viwanja vya CCM Ilomba ambapo Madee na TMK Wanaume Family wataimba.
Aliongeza kuwa Machi 15 itakuwa zamu ya Moshi na onesho litafanyikia katika kiwanja cha Majengo na wasanii watakaopanda jukwaani ni pamoja na Diamond,Joe Makini na Jambo Squad.
Njowoka alisema kuwa lengo kubwa na maonesho hayo ni kuwaweka karibu wananchi na kufurahia onesho la bure kutoka kwa wasanii wao.
"Najua kuwa hawa wasanii wanapendwa na washabiki wao ambao wengine hawana fedha za kulipia kuona shoo za wasanii hawa sasa tunawapatia fursa ya kuwaona bure kabisa"alisema Njowoka.
Aliongeza kuwa wasanii itakuwa ni fursa yao pia kuwa karibu zaidi na wapenzi wao wa burudani kuzungumza na na kuwa nao pamoja kama washabiki wao.
===========================