Mbeya City mdebwedo kwa Yanga
http://habari5.blogspot.com/2014/02/mbeya-city-mdebwedo-kwa-yanga.html
MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga jana walifanikiwa kuzima kasi na tambo za kutofungwa za mtimu ya Mbeya City baada ya kuizaba bao 1-0.
Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa kutokapa pand zote mbili ilishuhudia Yanga ikipoteza nafasi nyingi kupitia kwa chipukizi Simon Msuva na Davidi Luhenda licha ya kwenda mapunziko ikiwa mbele kwa bao hio moja lililofungwa na Mrisho Ngasa dakika ya 14.
Mbeya City ambayo iliingia katika mechi hiyo ikiwa imecheza mechi 15 za Ligi Kuu pasipo kutopeta mchezo hata mmoja jana ilijaribu marakadhaa kusawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji wake Mwagane Yeya na Paul Nonga lakini mipira waliyopiga ilidakwa na kipa wa Yanga Deogratius Munish na mengine kutoka nje.
Pamoja na kupata bao hilo la mapema Yanga iifanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 79 kupitia kwa Hamis Kiiza,lakini Mwamuzi Abdallah Kambuzi kutoka Shinyanga alilikataa kwa madai mfungaji alimsukuma beki wa Mbeya City.
Mwanzoni mwa kipindi cha pili Mbeya City, walijikuta wakicheza pungufu kufuatia kiungo wake Steven Mazanda kuonyesha kadi ya pili ya njano kufuatia kutoa luga ya matusi kwa Mwamuzi Kambuzi.
Yanga ambay licha ya ushindi huo wamesalia kwenye nafasi ya ili kufuatia Azam kuifunga Kagera Sugar mabao 4-0 kwenye mechi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chamazi Complex,iliendelea kuutawala mchezo huo kwa kutumia mapungufu ya Mbeya City lakini hawakuweza kubadili matokeo ya mchezo huo.
Zikiwa zimesawalia dakika tano mchezo huo kumalizika kiungo Athuman Idd ‘Chuji’,aliingia uwanjani na kuwaomba msamaha mashabiki wa Yanga kufuatia utovu wa nidhamu uliomsababisha kuwekwa pembeni na kukosa mechi tatu za ligi.
Pamoja na ushindani mkali uliokuwepo kwenye mechi hiyo timu zote zilionyesha kiwango cha juu kiasi cha kuwapa tumbo joto mashabiki matimu hizo ambao walijitokeza kwa wingi kuzishangilia timu zao.
Baada ya mchezo huo Jeshi la Polisi lilimkamata na kumfunga pingu mchezaji wa Yanga Shabani Kondo,ambaye hakucheza katika mchezo huo kwa madai ya kubishana na Askari mmoja akiwa anataka kuingia kwenye vyumba vya kuvalia wachezaji.
Kikosi cha kuzuia fujo uwanjani maarufu kama FFU,iliondoka uwanjani na mchezaji huyo ikiwa imempandisha kwenye gari yenye namba PT 2072.
MWISHO.