Sijapewa gari bure na Chief Kiumbe== Diamond
http://habari5.blogspot.com/2014/02/sijapewa-gari-bure-na-chif-kiumbe.html
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nasib Abdul, Diamond amekanusha kupewa gari bure na mdau wa muziki nchini Chief Kiumbe.
Diamond ambae anazidi kutamba na wimbo wake wa My Number One ambao pia ameurudia akiwa na msanii wa Nigeria Dovido anatajwa kuwa ni mmoja kati ya wasanii wa muziki wa Bongo Flavor ambao wanalipwa fedha nyingi katika shoo zake.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusiana na msanii huyo kuwa gari jipya analoendesha aina ya Toyota Land Cruiser V8 amezawadiwa na mdau huyo.
Akizungumza kwa niaba ya Diamond, Meneja wa wake Bob Tale alisema kuwa gari hilo Diamond amelinunua kutoka kwa Chief Kiumbe.
Tale alisema kuwa Diamond ameshalipia fedha za awali za ununuzi wa gari hilo ambapo hadi sasa ameshakamilisha asilimia 80 ya thamani ya gari zima.
Alisema kuwa msanii wake anashindwa kuelewa tuhuma za kupewa gari bure zinapotokea na ndio maana amekuwa akishindwa hata kujibu lolote kuhusiana na tuhuma hizo.
"Najua msanii kama Diamond ni mfano wa vijana wachakarikaji hapa mjini na ambao wamekuwa wakitumia nguvu zao kujipatia wanachotaka sasa ikianza kusemwa kuwa kapewa gari bure inaweza kuleta picha mbaya"alisema Tale.
Aliongeza kuwa walikaa kimya baada ya kuona kuwa hoja hiyo haina nguvu lakini wameshangaa kusikia kuwa hata mwenyewe Chif Kiumbe amekuwa akiendeleza maneno ya kutoa gari hilo bure.
Hivi majuzi katika gazeti pendwa moja ilitolewa picha ya Chif Kiumbe kurasa wa mbele wa gazeti hilo akisisitiza kuwa hakuwa na nia mbaya kwa kumzawadia gari hilo Diamond hatua ambayo imeonekana kumkera msanii huyo alieamua kufunguka kupitia meneja wake.