Simba yatua Morogoro tayari kuikabili Mtibwa kesho

WACHEZAJI wa Simba Nassor Chollo na Gilbert Kaze wataikosa mechi ya kesho kati ya  timu hiyo dhidi ya Mtibwa Sugar itakayofanyika katika uwanja wa Manungu mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Chollo anaikosa mechi hiyo kutokana na kuendelea na matibabu ya nyonga ya kushoto huku Kaze kwa upande wake anaendelea na matibabu ya goti
yanayomtaka kupumzika kwa wiki moja.

Akizungumzia mechi yao hiyo ya kesho Kocha Mkuu wa timu hiyo, Zdravko Logarusic alisema mbali na kuwakosa wacghezaji hao ana imani kuw akikosi chake kilichobakia kitaendelea kufanya vema.
Alisema kuwa wakiwa mkoani humo siku mbii kabla ya mechi watazoea hali ya hewa na hivyo kuwa tayari kupata ushindi hiyo kesho.
Alioneza kuwa kikosi chake kinaelekea mjini Morogoro wakitarajia kupanda upinzani kutoka kwa Mtibwa kwa vile kila timu inazihitaji pointi ili kuweza kujiimarisha katika msimamo wa ligi hiyo.

Alisema licha ya kutarajia upinzani ana matarajio makubwa ya ushindi katika mchezo huo kwa vile amekiandaa kikosi chake kwa ajili ya kupambana katika kutafuta ushindi.

"Wachezaji wapo salama na wapo katika hali ya ushindi tayari kwa kuvuna pointi hiyo kesho"alisema Loga.

Akizungumza na gazeti hili Msemaji wa Simba Asha Muhaji alisema kuwa mbali na wachezaji hao wawili kukosekana lakini timu hiyo imeondoka na wachezaji 22.

Alisema kuwa katika msafara wao huo pia wapo viongozi watano na wanatarajia kupiga kambi katika hoteli ya Mount Usambara kujiandaa na mpambano huo.

Asha alisema kuwa kikosi hicho kikiwa chini ya kocha wake Zdravko Logarusic kimeanza mazoezi katika Uwanja wa Jamhuri.

Asha alisema kuwa mchezaji Haruna Shamte aliyekuwa akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano atakuwemo katika msafara huo.

"Kwa timu hii imeondoka na wachezaji hao 22 na hadi sasa kimeshawasili mkoani humo salama tayari kwa kuachia kipigo hapo kesho"alisema Asha.

Naye Daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe alisema kuwa wachezaji wote wako katika hali nzuri kiafya kukiwa hakuna majeruhi hata mmoja.

Wachezaji walioondoka jana ni Ivo Mapunda, Yaw Berko, Abuu Hashim, William Lucian, Issa Rashid, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Awadh Juma, Amri Kiemba, Amisi Tambwe, Ramadhani Singano.

Wengine ni Henry Joseph, Abdulhalim Humud, Uhuru Selemani, Said Ndemla, Ramadhani Chombo, Gilbert Kaze, Haruna Shamte, Betram Mwombeki na Ali Badru. Makocha ni Logarusic, Selemani Matola, Idd Pazi, Meneja Nicco Nyagawa, Daktari Yassin Gembe na Mkuu wa Msafara ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Said Pamba. 

Related

Sticky 7418449485391876595

Post a Comment

emo-but-icon

item