Nyama Choma Festival we acha tu!!!

Hawa jamaa wa hili banda wao walionesha utaalamu wao wa aina hii


Mbuzi akiwa amening'inizwa

Hawa wadada walijiunda na kuchukua banda lao na kisha kutoa huduma kwa pamoja


Hawa jamaa walileta mbege yani ilikuwa poa sana

Unamkumbuka Victoria amekuwa mjasiliamali anauza juice ya matunda ni huyo amekaa chini hapo

Akiwa na kampani yake hapo

Wadau wa DSTV waliwakilisha, si unajua nyama  bia na kisha DSTV



Hawa ni wadau wa Wine ya Namaqua

Waliwakilisha vema walikuwa na wine nyingi za kuonjesha wadau

Waliwakilisha vema sana tena sana Wine zao ni poa kweli

Walipamba na staili flani za kiutamaduni kidogo na banda lao lilivutia sana

Wadau wa blogs walikuwapo huyo mzungu ni ndio mhusika mkuu wa hiyo Wine ya Amaqua akiwa na friends, mwenye draft ni Evance na wengine ni wadau wa GONGA IMX.

Mrembo akionesha Wine ya Namaqua

Nyomi kubwaa la watu




Kuna huyo jamaa alijitokeza na kutaka kumvalisha pete ya uchumba msanii kutoka Kenya aliepo hapa nchini Victoria Kimani lakini aliichomolea nje

Ilikuwa poa sana watu kibao, thanks kwa Carlo Ndosi kwa kubuni kitu kama hiki huo hiyo ndio ukisikia mtu kutumia fursa katika kujiingiza mkwanja kulikuwana watu kama zaidi ya elfu 8 hivi

Victoria akiwa amelakiwa na akinadada hawa, kwa wale wanaofuatilia muziki ni kwamba Victoria alizushiwa kuwa na uhusiano na msanii Diamond lakini alipofika tu hapa Dar aliakanusha kitu hicho lakini hat ahivyo alisema kuwa anawafagilia sana wanaume na wadada wa kibongo ile kusema hivyo ndo hawa wadada wakaenda kwanza jukwaani kumuonesha walivyojaliwa

Alipewa shangwe za kutosha huku Adama Mchomvu akiwa anamwimbisha jukwaani

Muziki ulikuwa safi huku kukiwa na sehemu moja ya muziki wa bendi ambapo Skylight waliwakilisha huku Ma dj wengine nao pia walifanya vitu vyao.

Related

Sticky 7699093818680740987

Post a Comment

emo-but-icon

item