Linah achukuliwa na NFK amaliza rasmi THT
http://habari5.blogspot.com/2014/07/linah-achukuliwa-na-nfk-amaliza-rasmi.html
Clouds na Linah |
Ruge akiwa na Ditto ambapo alimtunuku Ditto cheti ya kuwa mdau mahiri wa THT |
Pia Sheta alimwagiwa maji kibao kusherehekea kuzaliwa kwake hilo lilitokea hapohapo THT |
Hey huku hilo likiendelea Sheta akamwagiwa maji kusherehekea sikukuu yake |
Cloud alikuwapo pia kutoa pongezi zake |
Pia akatoa shukrani zake kwa Nkya |
Linah akamshukuru Mully B |
Hiyo nembo ya NFZ ni ina maana ya No Free Zone |
Linah akiingia |
Linah akiwa amepozi kwenye Red Carpet |
Wadau wa sanaa |
Wasanii wa Bongo Fleva walikuwapo pia |
Ruge akihutubia |
Pia iliendana sambamba na kukabidhi vyeti kwa wadau wa THT |
Lina akiwa na Meneja wake Abby |
Akampatia Mwasisi wa THT, Ruge Mutahaba zawadi ya kumshukuru kwa muda wote alipokuwa akifundishwa muziki na THT. |
KWA sasa wasanii wengi wa Tanzania wamekuwa wakijihusisha na utengenezaji wa video zao nje ya nchi huku wengi wakiwa wanaenda zaidi Afrika Kusini kutengeneza video zao hizo.
Wapo wasanii kama vile akina Diamond na Ommy Dimpoz ambao hao wote wametengeneza video zao Afrika Kusini ambapo Diamond alitengeneza ule wa My Number One na huku Ommy Dimpoz akifanya ule wa Baadae.
Mafanikio haya yanatokana na kuwa na uongozi mzuri kwa maana ya kuwa na menejimenti nzuri na yenye kujua nini inachokifanya.
Hilo limekuja kujitokeza kwa msanii Linah Sanga ambae ni hivi majuzi tu alitangaza kujiunga na kampuni mpya ya kusimamia kazi za sanaa kwa wasanii hapa nchini.
Kampuni hiyo aliyojiunga nayo inaitwa No Fake Zone, NFZ ambayo inamilikiwa na aliekuwa mshiriki wa shindano la Big Brother Africa mwaka 2006 Abby Plaatjes.
Linah ambae amekuzwa kimuziki akiwa na Tanzania House of Talent (THT) alipodumu kwa miaka saba kabla ya kuhamia kampuni hii mpya tayari ameshaanza kupanua shughuli zake za muziki.
Ameungana na wasanii wale ambao wanafanya kazi zao za sanaa nje ya Tanzania ambapo kwa upande wake ameshatengeneza video Afrika Kusini ya wimbo wake mpya uitwao Ole Themba.
Wimbo huo umetengenezwa na kampuni ya Gold Father ya Afrika Kusini ambapo ametumia takribani Milioni 50 kuutengeneza.
Akizungumza na gazeti hili, Lina anasema kuwa hatua aliyoifikia ni hatua ambayo anaiona kuwa inaelekea kumfikisha kwenye anga la kimataifa zaidi.
Anasema kuwa wimbo huo ulioandikwa na Mtayarishaji wa Muziki wa studio ya Soround Sound ya THT, Nash Designer ni wimbo ambao unamaadhi ya kiasilia huku ukiwa na kivutio kizuri.
Ni iwmbo ambao kiitikio chake kinavutia hata kwa watu ambao hawajui lugha ya kiswahili ila wanaweza kuuelewa wimbo huo na kiburudika nao.
Katika video ya wimbo huo anaonekana Linah akiwa amevalia nguo mchanganyiko zikiwamo zile za asili pamoja na za kisasa.
Inahusisha watu wa asili wakiwa wanacheza kiasili huku kukiwa na pia uhusishwaji kidogo wa mazingira ya vijijini.
Katika uzinduzi wa video hiyo uliofanyika kwenye kituo cha THT ulihudhuriwa na mamia ya wadau wa sanaa wakiwamo wasanii, watayarishaji wa muziki na wadau wengineo.
Katika hafla hiyo ambayo iliendana na futari ya pamoja Linah aliandaliwa maandalizi mazuri ya kumwaga THT pamoja na uzinduzi wa Video yake hiyo.
Huku kukiwa na wasanii wa filamu wa Bongo Movie pamoja na wasanii wengineo Linah hakusita kuelezea njia nzima kuanzia alivyoanza sanaa hiyo akijiunga na THT hadi alipopata dili la kuhamia kampuni ya No Fake Zone.
Anasema kuwa amekuwa kwenye sanaa ya muziki kwa muda huku akituimia muda mrefu zaidi kujifunza muziki na matumizi yake ya vifaa vya muziki.
Anaongeza kuwa amesoma muziki akiwa na THT na kisha kuanza kuimba akiwa na kituo hicho ambacho kimetoa mafunzo ya muziki kwa wasanii zaidi ya 300 hadi sasa.
"Muziki ni kazi yangu na kama ilivyo kwa kazi nyingine mtu anahama kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine na ndio ambavyo imetokea kwangu mimi nimetoka hapa THT ambapo nimekuza kipaji changu na ninahamia kwa No Fake Zone lakini bado nitakumbuka hapa THT kwa hali na mali"anasema Linah.
Linah alikabidhi zawadi kwa watu mbalimbali waliomsaidia kukuza kipaji chake ambapo aliwakabidhi zawadi ikiwa ni inshara ya kutambua mchango wao. Lakini Linah anaonekana ni wazi kuwa amevutiwa na mambo mengi kwenye wimbo huo kama vile Video yake hiyo wimbo wenyewe pamoja na kuwa na usimamiz wake mpya wa kampuni hiyo ya No Fake Zone.
Lina anaelezea furaha yake hiyo kuwa ni hatua moja kwenda nyingine ambapo kwa sasa anakuwa na usimamizi mpya wa kazi zake za sanaa.
Kwa upande wake mwasisi wa THT, Ruge Mutahaba anasema kuwa kilichofanyika kwa Linah ni inashara nzuri ya kukua kwa muziki wa Bongo Fleva hapa nchini.
Anaongeza kuwa hatua ya kampuni ya No Fake Zone kumchukua Linah ni sawa na mwanafunzi anapomaliza chuo na kuanza kazi kwa kuwa THT ni chuo tu cha
"Najua THT hapa ni chuo yani watu wanafundishwa muziki, wanatafutwa na kuelekezwa kila kitu kuhusiana na muziki na kwa wale ambao wanatoka na kupata kwengineko ni vema zaidi kwa kuwa hicho ndio tunachokitaka"anasema Ruge.
Ruge sio tu anamkaribisha tena Linah kituoni hapo bali pia anawakaribisha wasanii wengine wote waliowahi kupitia THT na hata wale ambao hawajawahi kuwa kituoni hapo.
Anasema kuwa THT kikiwa kituo chenye vyombo vya muziki, studio ya kurekodia pamoja na wataalamu kadhaa wa muziki wapo wasanii wengi ambao wanafika kupata huduma moja au nyingine.
"Najua muziki umekuwa na unazidi kukua kuna mengi ambayo sasa yanafanyika kwa faida zaidi, sasa wasanii wanatengeneza video zenye akili zaidi hii ni inshara kuwa muziki unalipa"anasema Ruge.
Ruge anatumia fursa hiyo kutambua nafasi za wasanii ambao kwa namna moja au nyingine wanajishughulisha na THT ambao ni Mwasiti, Hamadi Ayi, Imma the Boy, Ditto na Musa Savale.
Gazeti hili lilizungumza na mmoja kati ya wasanii waliohudhuria siku hiyo ambapo Mrisho Mpoto anasema kuwa hatua ya Linah kutengeneza video hiyo ya aina yake yenye asili ya kitanzania inaleta picha nzuri.
Anasema kuwa wasanii wengi wamekuwa wakitengeneza video zenye vionji vya ulaya zaidi lakini kwa alichokifanya Linah kimerejesha heshima ya muziki wa asilia pia.
"Najua wasanii hawa wanaitanga za nchi mimi ninampongeza sana tena sana tu kwa kuwa kile ambacho chini ya uongozi kampuni mpya wamekifanya na amenifungua macho kuhusiana na thamani ya sanaa hizi zenye vionjo vya asilia"anasema Mpoto.
Abby anasema kuwa kampuni yake hiyo imeanza kufanya kazi na Linah na lengo lake ni kuhakikisha kuwa muziki wa Bongo Fleva unavukia mipaka na kuwakilisha wasanii kimataifa.
Anaongeza kuwa wataendelea kusaidia muziki wa Bongo Fleva kwa kuwaandalia wasanii mazingira ya kufanya vema zaidi kama walivyaoanza kwa Linah kwa mkataba wa miaka miwili.
"Tumewekeza kwenye muziki kwa kuwa unalipa na kisha ndio mahala ambapo hata Tanzania inaweza kujitangaza zaidi na zaidi kupitia fani hii"anasema Abby.