Kansiime kufanya vitu vyake kesho Golden Tulip
http://habari5.blogspot.com/2014/08/kansiime-kufanya-vitu-vyake-kesho.html
MAKAMPUNI binafsi pamoja na idara za serikali katika nchi za Afrika Mashariki zimeombwa kusaidia ukuaji wa sanaa za vichekesho katika nchi zao.
Wito huo ulitolewa jana na mchekeshaji maarufu wa Uganda, Anne Kansiime wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na shoo yake anayoifanya leo katika hoteli ya Golden Tulip, Dar es salaam.
Alisema kuwa kupitia sekta ya vichekesho wananchi wanaweza kufikishwa kwa urahisi ujumbe kuhusiana na suala zima la amani na masuala mengine muhimu.
Alisema kuwa sanaa hiyo ni rahisi kufikisha ujumbe ambapo wasanii wanatimiza adhma yao hiyo huku wakiwa wanawafurahisha wananchi.
Alisema kuwa katika Jumuia ya Afrika Mashariki kuna mengi ya kujadiliwa ambapo sanaa hiyo inawezafanya.
"Tanzania nimepapenda sana na hii ikiwa ni mara yangu ya kwanza kuja nimependa sio tu nilivyopokelewa bali hata inavyoonekana kuipenda sanaa hiii na inatakiwa tuikuze kwa pamoja"alisema msanii huyo.
Kwa upande wake MC Pilipili mbali na kuwavunja mbavu waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo lakini pia aliwataka wachekeshaji kutokwamizwa na lugha ya Kiingereza katika kutanua shughuli zao za sanaa hiyo kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki.
"Wachekeshaji wa hapa nchini zamani tulikuwa tukichukuliwa ni kama vile watu wa kawaida kabisa na tusiokuwa na maana lakini kwa sasa tumefikia hatua ya watu kutukubali na tunatakiwa kujitambua na kujiendeleza"alisema Mc Pilipili.
Pia katika onesho hilo litahudhuriwa na mchekeshaji kutoka Kenya pia Fred Omondi.